Clicks49
sw.news

SSSPX: Uasi Kati Ya Waaminifu Paris

Mnamo tarehe kumi Jumuiya ya Mtakatifu Pius wa Kumi (SSPX) iliwaachisha kazi Mapadre wanane wa wilaya ya Ufaransa kwa sababu ya kutia saini kauli ambayo ni muhimu sana kwa nafasi ya Jumuiya ya SSPX kuhusiana na utambuzi wa Ndoa za wanaSSPX na Vatikani. Miongoni mwao alikuwa Padre Patrick de la Rocque, ambaye kufikia wakati huo alikua Padre msimamizi wa Paroko ya Mtakatifu Nicolas du Chardonet, Paris, paroko ya Jumuiya hiyo iliyo kubwa zaidi.

Jumapili iliyopita kabla ya hotuba yake, mkuu wa Wilaya ya Kifaransa, Padre Christian Bouchacourt, alisoma ujumbe katika Kanisa la Mtakatifu Nicolas huku akiitetea mikakati hiyo. Alipokua akiongea, takriban theluthi au nusu ya umati uliondoka kanisani kama ishara ya ukinzani, kulingana na contre-info.com. Wengine kadhaa walianza kuimba Rozali chini ya Mimbari, jambo ambalo lilisababisha mgogoro mdogo.

Kulingana na contre-info.com pengo lililo kati ya uongozi wa Jumuiya ya Mtakatifu Pius wa Kumi na Makakasisi wake wa Ufaransa, ambalo kwa kiasi kikubwa husababisha uhasama mkubwa dhidi ya upatanisho usio wa kimaadili na Urumi, bado linaonekana kukita mizizi.

Picha: Saint Nicolas du Chardonnet, © Tales of a Wanderer, Flickr, CC BY-NC, #newsGgozdanzye