sw.news
53

Itikadi Za Ushoga Ni Mwongozo Wa Kushindwa

Kanisa la kievanjelisti la shirika la Franklin, GracePointe, mjini Tennessee, lilisifiwa miaka miwili iliyopita kwa kukumbatia itikadi za ushoga. Pasta Stan Mitchell pia alimiminjwa sifa si haba kwenye gazeti la Times Magazine.

Hata hivyo, nusu ya waumini 2,200 waliondoka ghafla kutoka kwenye kanisa hilo baada ya tangazo hilo la ushoga. Sasa, hali halisi ya GracePointe imo hatarini. Mgeni aliyehudhuri ibada alihesabu takriban waumini 240 waliokuwa wamehudhuria, ambayo ni sehemu ndogo tu ya idadi iliyohudhuria hapo awali.

Hivyo basi Kanisa la GracePointe lilikodisha mali yakee kwa kikundi cha kievanjelisti kiitwacho Evangelical Group Cross Point ambacho husema kujihusu, "Huku huduma ya Cross Point ikiwa bunifu, tunachokiamini kumhusu Mungu sio. Imani yetu kuu humakinika na Kristo na ujumbe wake kama unavyopatikana kwenye Biblia."

Kituo cha Protestant Aquila Report kilitoa maoni, "Kumwondokea Yesu hakusaidii kukua kwa Kansia. Badala yake, hukweza kifo cha Kanisa." Papa Francis anafaa kulikumbuka hili.

Picha: © Mor, Flickr, CC BY-NC, #newsKgacdbgycf