sw.news
60

Muujiza: Padre Aliyetekwa Nyara Aachiliwa Huru

Miezi 18 baada yake kutekwa nyara, Padre wa Salesian Tom Uzhannalil, aliachiliwa huru na waliokuwa wamemteka nyara. Mnamo mwezi wa Machi mwaka wa 2016 mjini Aden, nchini Yemen, watu kumi na sita waliuawa …Zaidi
Miezi 18 baada yake kutekwa nyara, Padre wa Salesian Tom Uzhannalil, aliachiliwa huru na waliokuwa wamemteka nyara.
Mnamo mwezi wa Machi mwaka wa 2016 mjini Aden, nchini Yemen, watu kumi na sita waliuawa na wanamgambo wa kiislamu katika makao ya wazee ambayo hudhaminiwa na Wamisonari wa kutoa msaada. Miongoni mwa waliouawa ni watawa wanne Wamisonari: Watawa Marguerite na Reginette kutoka Rwanda, Mtawa Anselm kutoka India na mtawa Judit kutoka Kenya. Uzhunnalil ambaye alikuwa mkuu wa watawa hao, alichukuliwa mateka na wavamizi hao.
Waziri wa Masuala ya Mataifa ya Kigeni wa India, alitangaza siku ya Jumanne kupitia kwenye mtandao wa Twitter kuwa sasa Uzhannalil yuko Muscat, Oman, akijitayarisha kurejea India.
#newsBwbulhgbqp