Lugha
Mibofyo
39
sw.news

Maaskofu Watatu Wa Khazakhstan Wamkabili Papa Francis

Idhini yake Papa Francis kwa tamaduni za kichungaji za Maaskofu wa Buenos Aires imesababisha mtafaruku mwingi miongoni mwa waumini na wachungaji, kama walivyoandika maaskofu watatu wa Kazakhstan.

Maaskofu hao ni Askofu Mkuu wa Astana Tomash Peta, Askofu Mkuu wa Karaganda Jan Pawel Lenga na Askofu msaidizi wa Astana Athanasius Schneider. Kaulinyao hiyo ni ya mnamo tarehe Desemba 31, mwaka wa 2017.

Kauli hiyo inaziona tamaduni hizo za kichungaji kama mbinu ya kueneza "janva la talaka" hata katika maisha ya Kanisa. Uhalalishajinwa ndoa ya pili "kunawakilisha mabadiliko makuu katika tamaduni za kisakramenti zenye umri wa miaka elfu mbili" na mafundisho ya Kanisa.

Maaskofu hao huwanukuu mababa wa Kanisa kufikia hivi maajuzi ambao hukubaliana kwa mwito mmoja kiwa ndoa ya pili.

Wanatamatisha kuwa, "sio vyema kuhalalisha, kuidhinisha, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, talaka na ndoa zisizo dhabiti kingono kupitia tamaduni za kisakramenti ya kuwaalika waitwao "watalakiwa na waliofunga ndoa tena" katika Ekaristi Takatifu. Katika hali hii tamaduni za kigeni kwa Tamaduni zote za imani ya Kitume ya Kanisa Katoliki."

Picha: Tomash Peta, Jan Pawel Lenga, Athanasius Schneider, © wikicommons, CC BY-SA, #newsAamidgljnm
sw.news ametaja chapisho hili kwenye Askofu, Kanisa Linakumbwa Na "Utata Mkuu".