sw.news
83

Kasisi Wa Opus Dei, "John Paul II Aliyaona Majeshi Ya Kiislamu Yakivamia Uropa"

John Paul II alikuwa na maono makuu kuhusu Uislamu kulingana na Monsignor wa Opus Dei Mauro Longhi, mwenye umri wa miaka 68, aliyekuwa afisa katika Shirika la Wachungaji. Tangu mwaka wa 1985 hadi mwaka …Zaidi
John Paul II alikuwa na maono makuu kuhusu Uislamu kulingana na Monsignor wa Opus Dei Mauro Longhi, mwenye umri wa miaka 68, aliyekuwa afisa katika Shirika la Wachungaji. Tangu mwaka wa 1985 hadi mwaka wa 1995 Longhi alijiunga na John Paul II wakati wa likizo huko Abruzzo. Longhi anaamini kuwa John Paul II alikuwa mwenye maono.
Katika video iliyochaoishwa na Eventi per Famiglie Longhi anasema kuwa manamo mwezi Machi mwaka wa 1993 John Paul II alimwambia kuhusu maono aliyokuwa nayo: "Naliona Kanisa la milenia ya tatu likisumbuliwa na donda kuu liitwalo Uislamu. Watavamia Uropa. Niliona majeshi yakiwasili kutoka Magharibi yakielekea Mashariki, kutoka Morocco kwenda Libya, kutoka Misri kwenda kwa mataifa ya Mashariki."
Maelezo ya Longhi hayawezi kutegemewa kwa ukamilifu. "Majeshi ya Kiislamu" sio maneno yaliyoko kwenye msamiati wa John Paul II ambaye mnamo mwaka wa 1999 alibusu Korani na mnamo mwaka wa 2000 alifanya ombi kwa Mtakatifu John Baptist awalinde Waislamu.
#newsKmkpanoyap