sw.news
75

Watawa Wawili Wafariki Kwenye Ajali Mbaya Ya Barabarani Nchini Brazil

Ajali ya barabarani ilisababisha vifo vya Mtawa Giuseppina Lupo (37) wa kutoka Italia na Mtawa Luiza Manuel (46) wa kutoka Msumbiji (Mozambique). Wote wawili walikuwa wa shirika la Watawa wa Misionari Comboni na walikuwa wakifanya kazi katika Paroko ya Kikatoliki ya Santo Antônio do Matupi, Brazil.

Jumamosi asubuhi gari lao aina ya Mitsubishi Triton L200, lililokuwa likija kwa mwendo wa chini kutoka Santo Antônio do Matupi, lilipoteza mwelekeo na kubingiria. Watawa hao wawili walitupwa nje ya gari hilo na kufariki papo hapo. Walipatikana na wafanyakazi wa barabara.

Picha: Screenshot portalcm7.com, #newsOakxdczzds