Clicks322
sw.news

Kadinali Burke Mjini Bartislava: Shambulizi Kali Dhidi Ya Kanisa Hutoka Hadi "Kichwani Mwake"

Maadui wa Kanisa wanafurahia "Mashambulizi kali yaliyomo" dhidi ya mamlaka takatifu ya Kanisa kutoka ndani yake na "hata katika kichwa chake", Kadinali Raymond Burke aliambia umati mjini Bratislava, Slovakia (Aprili 27).

Akizungumza katika sherehe ya Bratislavské Hanusove Dni kuhusu ndoa na familia, alisema kwamba maadui wa Kanisa huwa hawakiri furaha yao hadharani ili watu wenye akili njema [wajinga] wasigundue kinachofanyika "hadi wakati ambapo uharibifu utakapokamilika."

Hivyo basi, Burke aliwahimiza Wakatoliki "kuendelea" kuulinda ukweli, "Hakuwezi kuwa na nafasi ya kimya na mtazamo wa kushindwa."

Alisema kwamba "utata na makosa" kuhusiana na ndoa ya Kikatoliki ziliibuliwa kwa mara ya kwanza na Kadinali Kasper. Hili "lilidhihirika machoni mwa ulimwengu wakati wa Sinodi la kwanza la Maaskofu mnamo mwaka wa 2014."

Burke alidhibitisha kwamba kuwapa wazini Ekaristi "kunahitilafiana na mafundisho dhabiti na vitendo vya Kanisa kuhusiana na ndoa takatifu".

Picha: Raymond Burke, #newsXchqtlcgub