Clicks52
sw.news

Habari Zinazochipuka: Vatikani Yapiga Marufuku Ekaristi Kwa Waprotesanti Nchini Ujerumani.

Shirika la Mafundisho ya Imani limetupilia mbali mpango wa Maaskofu Wajerumani kuwakubalisha Waprotestanti kupokea Ekaristi Takatifu, mtandao wa kath.net (Aprili 18) umeripoti.

Maaskofu hao walipiga kura mnamo mwezi Februari na kuunga mkono dhabihu hilo kwa njia ya walio wengi.

Hata hivo, Maaskofu saba walitilia shaka uamuzi huo huko Vatikani.

Sasa Shirika hilo limetupilia mbali dhana hiyo ya Wajerumani hao kwa idhin ya Papa Francis. Uamuzi huo mbaya tayari umetumwa kwa Maaskofu hao Wajerumani.

Hili ni pigo kuu kwa Kadinali wa Munich Reinhard Marx, Rais wa Baraza la Maaskofu hao na mwanachaa katika Baraza la Makadinali la Papa Francis.

Picha: © Mazur, catholicnews.org.uk, CC BY-NC-SA, #newsUoqrfhcceo