Clicks315
sw.news

Utengano Kati ya Francis Na Maaskofu Waholanzi

Maaskofu Waholanzi "hubadilika na kuwa friji kila wakati jina [Francis] linapotajwa", kulingana na Jan-Willem Wits, msemaji wa zamani wa Baraza la Maaskofu Waholanzi.

Akiandika kwenye mtandao wa blendle.com (Aprili 24), Wits alisema kwamba "watu Waholanzi" [husoma: vyombo vya habari visemavyo havina habari za Mungu] humpenda Francis- kinyume na Maaskofu [ambao huliongoza Kanisa ambalo lilibashiri itikadi za Bergoglio and hivyo basi, leo hii, limepungua kuwa vichane].

Kulingana na Wits Maaskofu hao Waholanzi wanadhani kwamba Francis "hupendekeza itikadi za kidemokrasia", ambaye hutaka "kuuza" ukweli wa milele wa Kanisa.

Wits alidai kwamba dhana ya kumwalika Francis nchini Uholanzi ilikataliwa na Waaskofu kwa sababu ya "ratiba yao iliyoshikamana".

Kufikia Baraza la pili la Vatikani, Kanisa nchini Uholanzi lilikuwa ngome kuu ya Katoliki. Baada ya Baraza hilo, lilichukuliwa kuwa katika mstari wa mbele wa "ukarabati" uliotakikana na Baraza hilo lakini "ukarabati" huu ulitamatika kwa janga.

Katika miaka kumi iliyopita zaidi ya Makanisa 1000 ya Katoliki yamefungwa. Leo hii, waumini nchini Uholanzi ni vikundi vidogo sana, vikihusisha haswa wahamaji.

Picha: © Mazur, catholicchurch.org.uk, CC BY-NC-SA, #newsHkqxgbjyhx