sw.news
sw.news
473

Kadinali Burke Mjini Bartislava: Shambulizi Kali Dhidi Ya Kanisa Hutoka Hadi "Kichwani Mwake"

Maadui wa Kanisa wanafurahia "Mashambulizi kali yaliyomo" dhidi ya mamlaka takatifu ya Kanisa kutoka ndani yake na "hata katika kichwa chake", Kadinali Raymond Burke aliambia umati mjini Bratislava, …Zaidi
Maadui wa Kanisa wanafurahia "Mashambulizi kali yaliyomo" dhidi ya mamlaka takatifu ya Kanisa kutoka ndani yake na "hata katika kichwa chake", Kadinali Raymond Burke aliambia umati mjini Bratislava, Slovakia (Aprili 27).
Akizungumza katika sherehe ya Bratislavské Hanusove Dni kuhusu ndoa na familia, alisema kwamba maadui wa Kanisa huwa hawakiri furaha yao hadharani ili watu wenye akili njema [wajinga] wasigundue kinachofanyika "hadi wakati ambapo uharibifu utakapokamilika."
Hivyo basi, Burke aliwahimiza Wakatoliki "kuendelea" kuulinda ukweli, "Hakuwezi kuwa na nafasi ya kimya na mtazamo wa kushindwa."
Alisema kwamba "utata na makosa" kuhusiana na ndoa ya Kikatoliki ziliibuliwa kwa mara ya kwanza na Kadinali Kasper. Hili "lilidhihirika machoni mwa ulimwengu wakati wa Sinodi la kwanza la Maaskofu mnamo mwaka wa 2014."
Burke alidhibitisha kwamba kuwapa wazini Ekaristi "kunahitilafiana na mafundisho dhabiti na vitendo vya Kanisa kuhusiana na ndoa takatifu".
Picha: Raymond Burke, #newsXchqtlcgub
sw.news
473

Kadinali Marx Apingaye Kanisa Apigana Dhidi Ya Msalaba

Kadinali wa Munich ambaye hulipinga Kanisa Reinhard Marx, akizungumza na jarida linalomilikiwa na matajiri wenye ushawishi mkuu serikalini Süddeutsche alikashifu kwa mara nyingine uamuzi wa Waziri …Zaidi
Kadinali wa Munich ambaye hulipinga Kanisa Reinhard Marx, akizungumza na jarida linalomilikiwa na matajiri wenye ushawishi mkuu serikalini Süddeutsche alikashifu kwa mara nyingine uamuzi wa Waziri mkuu Markus Söder wa Bavaria, Ujerumani, kubandika misalaba katika nyumba zote za umma.
Kulingana na Marx, uamuzi huu umesababisha "utengano, msukosuko, mzozo" - kana kwamba msalaba umewahi kusababisha jambo lingine.
Alimaanisha kwamba msalaba ulitumika "tu" kama ishara ya mila na kwamba kwa njia hii msalaba "unanyang'anywa kwa jina la taifa".
Katibu mkuu wa CSU, chama cha walio wengi huko Bavaria, alisema kwamba wanaoukosoa uamuzi huo ni "jumuiya ovu ya maadui wa dini na wasiojikubali".
Picha: Reinhard Marx, © Maik Meid, CC BY-SA, #newsXtgjuvovzq
sw.news
473

Marafiki Wa Kushangaza: Francis Akutana Na Mtetezi Wa Ushoga Na Uavyaji Mimba Kate Perry

Mwanamuziki Mmarekani aitwaye Katy perry, 33, alizungumza katika kongamano la Vatikani la "United to Cure", ambalo liliandaliwa na Baraza la Upapa la Tamaduni kuanzia Aprili tarehe 26 hadi 28. Mnamo …Zaidi
Mwanamuziki Mmarekani aitwaye Katy perry, 33, alizungumza katika kongamano la Vatikani la "United to Cure", ambalo liliandaliwa na Baraza la Upapa la Tamaduni kuanzia Aprili tarehe 26 hadi 28.
Mnamo siku ya Jumamosi, Papa Francis alimpokea pamoja na mwigizaji Orlando Bloom, 41, ambaye wanaishi pamoja na Perry kwa sasa.
Perry alijieleza kama "mtetezi wa haki za "wanawake" na "mwanaharakati wa ushoga", na amepokea tuzi nyingi za kishoga. Perry alicheza katika sherehe kadhaa wakati wa kampeni za urais za Hillary Clinton ambaye huunga mkono uavyaji mimba.
Mwanamuziki huyo aliyejawa na utata alihusika katika ubishi mkali wa kisheria na Watawa wa Bikra Maria wa Roho ya Maria mjini Los Angeles ambao walitaka kumzuia Perry dhidi ya kununua moja ya mali yao. Mmoja wa watawa hao, Mtawa Catherine Holzman, 89, alifariki wakati wa kesi hiyo mahakamani.
Miaka kadhaa iliyopita Perry alisema kwenye mahojiano ya video kwamba, "Niliuuza moyo wangu kwa shetani."
Mnamo mwaka wa 2016 alichanga Dola 10,000…Zaidi
sw.news
455

Kadinali Wa Francis Amlinda Askofu Msaidizi Anayekumbwa Na Utata

Askofu msaidizi Juan Pineda wa Tegucigalpa, Honduras, juishi maisha ya kifahari ambayo huhusisha umiliki wa magari kadhaa ya kifahari na safari za mara kwa mara za ndege za kifahari, Edward Pentin …Zaidi
Askofu msaidizi Juan Pineda wa Tegucigalpa, Honduras, juishi maisha ya kifahari ambayo huhusisha umiliki wa magari kadhaa ya kifahari na safari za mara kwa mara za ndege za kifahari, Edward Pentin aliripoti (Aprili 27).
Hata hivyo, Pineda hubaki katika wadhfa wake kwa ulinzi wake Kadinali wa Tegucigalpa Oscar Rodríguez Maradiaga, rafiki wa karibu wa Pineda ambaye pia ni mratibu wa Baraza la Makadinali na mwanapropaganda wa itikadi za "ufukara" za Francis.
Kulingana na Pentin, Pineda alihusika katika kutoweka kwa Dola milioni 1.3 ambazo zilitolewa na serikali ya Hondura kwa miradi ya msaada ya Kanisa. Fedha hizo ziliwekwa ila hazikupitia utaratibu wa kawaida wa kifedha wa dayosisi hiyo na hatimaye "zikatoweka".
Pineda alijaribu kueleza zilivotumika pesa hizo, lakini ripoti yake haikutoa hati za invoisi, vocha wala hati zozote.
Mwezi uliopita, Pentin alifichua kwamba Pineda amekashifiwa na wanaseminari wa zamani kwa shutma za dhulma za kishoga.
Picha: Juan Pineda, © House Committee on …Zaidi
sw.news
442

Marekebisho Ya Fedha Za Vatikani Yashuhudia "Kinyume Halisi"

Mtaalamu ambaye hajatambulishwa alimwambia Edward Pentin (Aprili 27) kwamba marekebisho yanayosemekana ya Fedha za Vatikani yamefeli. Kulingana naye, kesi kadhaa za jinai za kifedha zilifichuliwa katika …Zaidi
Mtaalamu ambaye hajatambulishwa alimwambia Edward Pentin (Aprili 27) kwamba marekebisho yanayosemekana ya Fedha za Vatikani yamefeli.
Kulingana naye, kesi kadhaa za jinai za kifedha zilifichuliwa katika miaka ya kwanza ya upapa wa Francis, ila hayakushtakiwa.
Afisi ya "Mfadhili wa Haki" huchagua kesi chache tu huku ikizipuuza zingine.
Msemaji huyo aliongeza kuwa, "Ingawaje hakuna mtu anayetaka kukiri jambo hili, kwa ufanisi tunashuhudia kinyume cha utaratibu wa marekebisho ya miaka mitano iliyopita."
Picha: © European Parliament, CC BY-NC-ND, #newsZkjlvceinz
sw.news
440

Mdahalo: Francis Auita Uaminifu "Uthabiti"

Papa Francis alishiriki mnamo tarehe 24 mwezi Aprili Ibada mpya huko Santa Malta pamoja na Makadinali tisa ambao ni wanachama wa baraza lake. Katika hotuba yake, Francis aliwatukanatena "madaktari wa …Zaidi
Papa Francis alishiriki mnamo tarehe 24 mwezi Aprili Ibada mpya huko Santa Malta pamoja na Makadinali tisa ambao ni wanachama wa baraza lake.
Katika hotuba yake, Francis aliwatukanatena "madaktari wa sheria" huku akiukana "uthabiti" wao na "upinzani kwa dhana mpya".
Kisha alilalamika kwamba kuna "upinzani dhidi ya mambo mapya na mabadiliko".
Mdahalo wa Francis ulikumbusha kuhusu propaganda dhidi ya Kansia katoliki mitaani ambazo hupuuza uaminifu kama "uthabiti" na dhana za kimantiki kama "upinzani dhidi ya mambo mapya". wakati huo huo uzushi unaitwa "mabadiliko" na kuangamia katika makosa ya kitambo kama "mambo mapya".
#newsMdyfyscafy
sw.news
435

Utengano Kati ya Francis Na Maaskofu Waholanzi

Maaskofu Waholanzi "hubadilika na kuwa friji kila wakati jina [Francis] linapotajwa", kulingana na Jan-Willem Wits, msemaji wa zamani wa Baraza la Maaskofu Waholanzi. Akiandika kwenye mtandao wa Zaidi
Maaskofu Waholanzi "hubadilika na kuwa friji kila wakati jina [Francis] linapotajwa", kulingana na Jan-Willem Wits, msemaji wa zamani wa Baraza la Maaskofu Waholanzi.
Akiandika kwenye mtandao wa blendle.com (Aprili 24), Wits alisema kwamba "watu Waholanzi" [husoma: vyombo vya habari visemavyo havina habari za Mungu] humpenda Francis- kinyume na Maaskofu [ambao huliongoza Kanisa ambalo lilibashiri itikadi za Bergoglio and hivyo basi, leo hii, limepungua kuwa vichane].
Kulingana na Wits Maaskofu hao Waholanzi wanadhani kwamba Francis "hupendekeza itikadi za kidemokrasia", ambaye hutaka "kuuza" ukweli wa milele wa Kanisa.
Wits alidai kwamba dhana ya kumwalika Francis nchini Uholanzi ilikataliwa na Waaskofu kwa sababu ya "ratiba yao iliyoshikamana".
Kufikia Baraza la pili la Vatikani, Kanisa nchini Uholanzi lilikuwa ngome kuu ya Katoliki. Baada ya Baraza hilo, lilichukuliwa kuwa katika mstari wa mbele wa "ukarabati" uliotakikana na Baraza hilo lakini "ukarabati" huu ulitamatika kwa janga. …Zaidi
sw.news
444

Ukinzani Zaidi Kutoka Kwa Kasper: Waprotestanti Na Wakatoliki Ni "Kanisa Moja"

Akizungumza kwa ukinzani, Mprotestanti halisi Kadinali Walter Kasper amedai kwamba Wakatoliki na Waprotestanti ni wanachama wa "Kanisa moja Takatifu la Kristo" lakini wakati uo huo "sio katika ushirika …Zaidi
Akizungumza kwa ukinzani, Mprotestanti halisi Kadinali Walter Kasper amedai kwamba Wakatoliki na Waprotestanti ni wanachama wa "Kanisa moja Takatifu la Kristo" lakini wakati uo huo "sio katika ushirika kamili.
Akiandika kwenye mtandao wa katholisch.de (Aprili 23), Kasper aliliwacha wazi jinsi ambavyo mtu anaweza kuwa mwanachama wa mwili wa Kristo huku asipokuwa mwanachama kamili wa mwili huo.
Kaw msingi huu anaomba kuwe na Ekaristi kwa Waprotestanti, haswa kwa ndoa kati ya watu wa dini tofauti kwani husemekana kwamba wao huunda "kanisa la kinyumbani".
Lakini Kasper hajibu swali ni kwa nini Waprotestanti halisi wangetaka kupokea Ekaristi Takatifu. Au: Iwapo mtu asiye Mkatoliki ana mvuto wa kweli kwa Ekaristi ya Kikatoliki, ana wajibu wa kidini na kimaadili kujiunga na ushirika huu.
Kupokea Ekaristi huku akiukataa Ushirika kunakinzanam, hakumfai Mkristo ambaye ameitwa kuishi katika ukweli wa Kristo ambako hakuna ukinzani.
Picha: Walter Kasper, © Mazur, catholicchurch.org.uk, CC BY-NC-SAZaidi
sw.news
432

Upoli: Vifaa Vya Intaneti Vyawekwa Kwenye Sanamu Ya Yesu Kristo

Mojawapo ya sanamu refu zaidi duniani ya Yesu Kristo mjini Świebodzin, nchini Upoli, ina vifaa vya kiufundi ndani ya taji lililoko juu ya kichwa cha sanamu hiyo. Mtaalamu aliambia fakt.pl (Aprili 22…Zaidi
Mojawapo ya sanamu refu zaidi duniani ya Yesu Kristo mjini Świebodzin, nchini Upoli, ina vifaa vya kiufundi ndani ya taji lililoko juu ya kichwa cha sanamu hiyo.
Mtaalamu aliambia fakt.pl (Aprili 22) kwamba vifaa hivyo vinatumika katika usambazaji wa mitambo ya intaneti.
Parokia inayomiliki sanamu hiyo iliyoko vitongojini mwa mji huo ilikataa kutoa maoni.
Sanamu hiyo iliundwa kwa mwaada kutoka kwa wakaazi wa humo.
#newsTmfoevbtox
sw.news
438

Uropa Inakumbwa Na Upungufu Wa Idadi Ya Watu

"Kusipochukuliwa hatua kwa haraka sana, Bara Uropa limo katika hatari ya upungufu mkuu wa idadi ya watu" kulingana na Antoine Renard, rais wa shirika la Federation of Catholic Family Associations mjini …Zaidi
"Kusipochukuliwa hatua kwa haraka sana, Bara Uropa limo katika hatari ya upungufu mkuu wa idadi ya watu" kulingana na Antoine Renard, rais wa shirika la Federation of Catholic Family Associations mjini Brussels.
[Tayari ni wazi kuwa itikadi zinazotawala za vyama vingi dhidi ya familia hazitakubalisha kuchukuliwe hatua.]
Akizungumza na Catholic News Service (Aprili 19), Renard alitoa mwito kuwe na msaada wa kisiasa kuanzisha familia. Serikali zinastahili "kuweka familia katika kilele cha sera za kitaifa."
Muungano wa uropa ulikuwa na idadi ya uzazi ya 1,58 kwa kila mwanamke katika mwaka wa 2015. Kiwango cha ubadilishaji kingekuwa takriban uzazi wa 2.1 kwa kila mwanamke.
Wanasiasa waliofeli kama vile Angela Merkel hujaribu kuficha matokeo mabaya ya sera za familia kwa kuwaiba watu kutoka mataifa fukara, na kuyaondolea viijana wao na kusababisha janga la idadi ya watu huko pia.
Picha: © myri_bonnie, CC BY-NC-ND, #newsBadleqaodp
sw.news
447

Askofu Msiria: Ni Heri Syria Kuliko Na Vita Kushinda Uropa Iliyooza

Wasiria hawafai kuhama kwani hawata pata furaha barani Uropa, Askofu Mkatoliki wa Siria Jano Battah alisema. Akizungumza na Syriana Analysis (Aprili 12) Battah alisema kuna "maisha ya faraja" barani …Zaidi
Wasiria hawafai kuhama kwani hawata pata furaha barani Uropa, Askofu Mkatoliki wa Siria Jano Battah alisema.
Akizungumza na Syriana Analysis (Aprili 12) Battah alisema kuna "maisha ya faraja" barani Uropa. Lakini hili huja kwa dhamani, "Mapinduzi ya Ufaransa yamempuuza Mungu."
Battah ameishi Uropa kwa muda wa miaka 15 na anajua kwamba Wakristo barani Uropa ndio walio wachache. Nchini Ufaransa "asilimia ya watu ambao hawaamini uwepo wa Mungu ni nyingi zaidi".
Kuhusu siasa za Syria alisema, Kwamba hakuna hakuna mbadala ila Rais Assad, "Iwapo utachagua kati ya Assad na msitu, utamchagua Assad."
Kulingana na Battah "shida halisi ni sera mbaya za Marekani". Na, "Isingelikuwa ni Urusi, tayari tungekuwa tumechinjwa."
Battah anasema kwamba hakuna vita kati ya Wakristo na Waislamu nchini Syria.
ISIS "haina uhusiano na Uislamu" ila "ni chama cha kisiasa" na "kimetumwa kutoka nje."
Picha: Jano Battah, #newsIexnttxkjf
sw.news
425

Kadinali Müller Awakashifu Wanachama wa Pro-Life Ambao Hukosoa Mapendeleo Ya Papa Francis Ya Uavyaji Mimba

Wanaharakati wa Pro-life duniani kote wanamkashifu Papa Francis kwa kukadirisha uavyaji mimba kwa kuulinganisha na masuala ya haki za kijamii kama vile uhamaji na umaskini. Katika Mahimizo yake ya …Zaidi
Wanaharakati wa Pro-life duniani kote wanamkashifu Papa Francis kwa kukadirisha uavyaji mimba kwa kuulinganisha na masuala ya haki za kijamii kama vile uhamaji na umaskini.
Katika Mahimizo yake ya Kichungaji Gaudete et Exsultate, 101, Francis anadai kwamba maisha ya watu ambao wanateseka ni "takatifu" sawa na maisha ya watoto wasio na hatia huku akipuuza ukweli kuwa kuteseka na kuuawa sio sawa katika njia yoyote ile.
Huku akiendelea na mbinu yake ya kupindukapinduka Kadinali Gerhard Müller a akizungumza na mtandao wa lizikosoa sauti hizi NcRegister.com (Aprili 21). alidai kwamba ni "bila shaka vibaya kumjumuisha Francis kama mtangazaji wa itikadi za tamaduni mbaya za kifo".
Lakini ni ukweli kwamba Francis alimtunuku mnamo mwaka wa 2017 mwanasiasa Mholanzi Lilianne Ploumen, mwnezaji mkali wa propaganda za uavyaji mimba, na Daraja la Upapa la Mtakatifu Gregory.
Nchini Italia huwapendekeza watu kama vile Emma Bonino ambaye, licha ya kutokuwa daktari wa afya, alitekeleza uavyaji mimba …Zaidi
sw.news
128

Askofu Mwothodoksi Mgriki Huko Jerusalem Ahusika Katika Kashfa Na Shoga

Askofu Mwathodoksi Mgriki Isichios Kontogiannis wa Capitolias, Jordan, amejiondoa kwenye majukumu yake, baada ya kuonekana kwenye kanda ya video akishiriki katika vitendo vya ngono na mwanaume aliyekuwa …Zaidi
Askofu Mwathodoksi Mgriki Isichios Kontogiannis wa Capitolias, Jordan, amejiondoa kwenye majukumu yake, baada ya kuonekana kwenye kanda ya video akishiriki katika vitendo vya ngono na mwanaume aliyekuwa amevalia mavazi ya kike.
Askofu huyo alijihusisha na mwanaume Mgiriki ambaye hujiita "Afroditi Konstantinou". Alikuwa kahaba wa kishoga na huvlia mavazi ya kike. Kulingana naye uhusiano huo umekuwepo kwa zaidi ya miaka mitano.
Konstantinou alichapisha video za kutamausha kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuhisi kuwa "ametumiwa vibaya" kihisia na kudhulumiwa kimwili na kiakili
#newsTdpwwkabdl
sw.news
87

Ekaristi Kwa Waprotestanti: Kadinali Müller Amkosoa Kadinali Marx

Kadinali Gerhard Müller amesema katika mtandao wa firstthings.com (Aprili 20) kwamba Ekaristi katika Sakramenti haiwezi kutenganishwa na ushirika wa Kikanisa. Alimkashifu Kadinali wa Munich Reingard …Zaidi
Kadinali Gerhard Müller amesema katika mtandao wa firstthings.com (Aprili 20) kwamba Ekaristi katika Sakramenti haiwezi kutenganishwa na ushirika wa Kikanisa.
Alimkashifu Kadinali wa Munich Reingard Marx na mpango wake wa kuhalalisha Ekaristi kwa Waprotestanti jambo ambalo limekuwa la lazima nchni Ujerumani kwa miongo mingi.
Müller alimweleza Marx kwamba haiwezi kuwa kwamba Teolojia ya kimsingi husema hili, huku Teolojia ya uchungaji kufanya kinyume, "Kilicho makosa kimsingi kitakuwa na athari hatari katika kazi ya uchungaji hivi kwamba kazi ya uchungaji itakuwa ikielekezwa na kanuni bandia, na kuhatarisha ukombozi wa nyoyo."
Müller anahitimisha kwamba wala maskofu au Papa wana "ujuzi" wa kuingilia kati msingi wa Sakramenti.
Picha: Gerhard Ludwig Müller, Gustavo Gutierrez, #newsQrkpdfyxet
sw.news
100

Mpungaji Pepo Apendwaye Na Francis Ni "Mlutheri"

Profesa Giuseppe Ferrari, mwandalizi wa "Zamu ya Upungaji Pepo" ya kila mwaka katika Chuo kikuu cha Roma "Regina Apostolorum" ambacho kinamilikiwa na Maaskari wa Kristo, aliambia kituo cha habari bandia …Zaidi
Profesa Giuseppe Ferrari, mwandalizi wa "Zamu ya Upungaji Pepo" ya kila mwaka katika Chuo kikuu cha Roma "Regina Apostolorum" ambacho kinamilikiwa na Maaskari wa Kristo, aliambia kituo cha habari bandia New York Times (Aprili 19) kwamba katika kongamano la mwaka ujao anataka kualika "mpungaji peo anayependwa zaidi na Papa, Mlutheri".
Ferrari hakutaja jina lake.
Hata hivyo, mnamo mwezi Machi mwaka wa 2013 Mwajentina Diario Popular alimtangaza mhubiri wa Kilutheri Manuel Acuña kama "mpungaji pepo anayependwa zaidi na Papa Francis".
Acuña ambaye hujiita "Askofu" na huvalia mavazi kama ya Askofu Mkatoliki, ni rafiki wa karibu wa Fracis. Ni mwanahama wa "Kanisa la Karismatiki la Ajentina". Mnamo mwezi Machi mwaka wa 2015 "alipunga pepo" kutoka kwa mwanamke mwenye umri wa miaka 22 katika ibada iliyoprprushwa moja kwa moja. Mtandao wa Debate.com.mx uliita kipindi hicho cha moja kwa moja "cha kingono na kisicho cha kawaida".
Bergoglio alikuwa akimpendekeza Acuña kama mponyaji wa kiroho kila …Zaidi
sw.news
100

Askofu Wa Austria Ana Kasula Angavu

Jumba la Makumbusho la Makao ya Watawa ya Admont ya Wabenedikti, Austria, limeonyesha mali ya Askofu mpya wa Innsbruck, Hermann Glettler ambaye alitiwa wakfu mnamo mwezi Desemba mwaka wa 2017. Miongoni …Zaidi
Jumba la Makumbusho la Makao ya Watawa ya Admont ya Wabenedikti, Austria, limeonyesha mali ya Askofu mpya wa Innsbruck, Hermann Glettler ambaye alitiwa wakfu mnamo mwezi Desemba mwaka wa 2017.
Miongoni mwa mali hiyo ni picha ya mnamo mwaka wa 2004 ya Glettler akiwa amevalia "kasula" angavu iliyotengenezwa kwa plastiki. Picha hiyo pia imo kwenye ukurasa wa kwanza wa daftari ya jumba hilo la Makumbusho.
Gletter ana imani katika makasisi wa kike. Kuteuliwa kwake kulisifiwa kwa kina na vyombo vya habari.
#newsKjnocdvrkq
sw.news
96

Maaskofu Wajerumani: Papa Francis Hana Shida Na Ekaristi Kwa Waprotestanti

Msemaji wa maaskofu Wajerumani akiandika kwenye mtandao wa dbk.de (Aprili 19) amekana kwamba Vatikani ilitupilia mbali uamuzi wa maaskofu Wajerumani kuwapa Waprotestanti Ekaristi. Kulingana naye Zaidi
Msemaji wa maaskofu Wajerumani akiandika kwenye mtandao wa dbk.de (Aprili 19) amekana kwamba Vatikani ilitupilia mbali uamuzi wa maaskofu Wajerumani kuwapa Waprotestanti Ekaristi.
Kulingana naye repoti zinazotoa kauli tofauti, ni "zenye uongo".
Mkano huo unathiditisha kwamba Kadinali wa Munich Reinhard Marx atakutana na Papap Francis kulijadili suala hilo.
Matokeo ya mkutano huo yanaweza kutabiriwa: Francis atasababisha taharuki na kuvikubalisha vyama vyote kudai kwamba anaviunga mkono huku akikubali Ekaristi kwa Waprotestanti.
Ekaristi kwa Waprotestanti imedukizwa katika Kanisa "Katoliki" nchini Ujerumani kwa miongo mingi. Kasisi Mkatoliki ambaye angekataa kulifanya hili, hakueza kuushikilia wadhfa wake.
Picha: Reinhard Marx, © Maik Meid, CC BY-SA, #newsPkuvleqvdz
sw.news
91

Francis Alitaka Barua Iliyopiga Marufuku Ekaristi Kwa Waprotestanti Kuwa "Siri"

Edward Pentin alidhibitisha ripoti kwamba Shirika la Mafundisho ya Imani limetupilia mbali pendekezo la Maaskofu Wajerumani kuwapa Waprotestanti Ekaristi [ingawaje hili ni jambo la kawaida nchini humo]. …Zaidi
Edward Pentin alidhibitisha ripoti kwamba Shirika la Mafundisho ya Imani limetupilia mbali pendekezo la Maaskofu Wajerumani kuwapa Waprotestanti Ekaristi [ingawaje hili ni jambo la kawaida nchini humo].
Aliyempa Pentin habari hizo aliongeza kuhusu suala hili, hakuna "tofauti" kati ya Askofu Mkuu Ladaria na mtangulizi wake Kadinali Gerhard Müller.
Pentin amegubdua kwamba "Papa anaitaka barua [inayopiga marufuku pendekezo hilo] ibaki kuwa siri kwa sababu zisizojulikana".
Picha: © European Parliament, CC BY-NC-ND, #newsNmaxqrapam
sw.news
90

Muziki WA Litajia Ni Upanga Wenye Pande Mbili - Na Maestro Aurelio Porfiri

Muziki ni muhimu katika litajia na hivyo basi ni lazima uchukuliwa kwa umakinifu fulani. Wastaarabu wa zamani, haswa Wagriki, walielewa nguvu za muziki, na sayansi ya ubongo imethibitisha: muziki una …Zaidi
Muziki ni muhimu katika litajia na hivyo basi ni lazima uchukuliwa kwa umakinifu fulani.
Wastaarabu wa zamani, haswa Wagriki, walielewa nguvu za muziki, na sayansi ya ubongo imethibitisha: muziki una athari ya kina juu ya hisia zetu na jinsi tuyaonavyo mambo.
Lakini kinachoweza kuwa njiz kuu ya maombi na uhubiri kinaweza kubdilika na kuwa silaha hatari.
Kwa bahati mbaya, muziki wa sasa wa Litajia hutumika kwa mara nyingi kuwapendeza wanadunia, wala sio roho.
Uovu wa muziki wa kilitajia ni janga la nyakati zetu , sio tu kwa Wakatoliki tu lakini pia kwa utamaduni pia.
Iwapo muziki wa Kanisa utawapendeza wanadunia na kutotuinua juu ya kilicho cha kawaida tena, basi umefeli wajibu wake.
Huwa tunaitawala dunia au sdunia itutawale.
Muziki wa litajia ni silaha yenye nguvu, dhidi ya dunia au dhidi ya Kanisa. Aurelio Porfiri ni mtunzi , mwongozaji, mwalimu na mwandishi. Amechapisha zaidi ya nyimbo 100 nchini Italia, Ujerumani, Uchina,Marekani na Ufaransa, na takriban vitabu 30 na zaidi ya nakala …Zaidi
sw.news
99

Habari Zinazochipuka: Vatikani Yapiga Marufuku Ekaristi Kwa Waprotesanti Nchini Ujerumani.

Shirika la Mafundisho ya Imani limetupilia mbali mpango wa Maaskofu Wajerumani kuwakubalisha Waprotestanti kupokea Ekaristi Takatifu, mtandao wa kath.net (Aprili 18) umeripoti. Maaskofu hao walipiga kuraZaidi
Shirika la Mafundisho ya Imani limetupilia mbali mpango wa Maaskofu Wajerumani kuwakubalisha Waprotestanti kupokea Ekaristi Takatifu, mtandao wa kath.net (Aprili 18) umeripoti.
Maaskofu hao walipiga kura mnamo mwezi Februari na kuunga mkono dhabihu hilo kwa njia ya walio wengi.
Hata hivo, Maaskofu saba walitilia shaka uamuzi huo huko Vatikani.
Sasa Shirika hilo limetupilia mbali dhana hiyo ya Wajerumani hao kwa idhin ya Papa Francis. Uamuzi huo mbaya tayari umetumwa kwa Maaskofu hao Wajerumani.
Hili ni pigo kuu kwa Kadinali wa Munich Reinhard Marx, Rais wa Baraza la Maaskofu hao na mwanachaa katika Baraza la Makadinali la Papa Francis.
Picha: © Mazur, catholicnews.org.uk, CC BY-NC-SA, #newsUoqrfhcceo