sw.news
69

"Padre Euro" Ahusika Na Kashfa Ya Ukahaba Wa Kishoga

Viongozi wa mashtaka huko Massa Carrara, nchini Italia, wameanzisha upelelezi dhidi ya Padre Luca Morini kwa madai ya "kutumia kwa njia isiyo halali pesa za dayosisi hiyo" na "jaribio la ulaghai". Walishika Uro 700,000 pesa taslimu na dhamana ya Uro 150,000 katika mawe ya thamani na hisa kutoka kwa Padre huyo.

Morini alizitumia pesa hizo kufadhili maisha ya kishoga. Kahaba mwanaume mwenye wivu amabaye hapo awali alimchukulia padre huyo kuwa Hakimu tajiri, alirekodi sherehe za kishoga, zawadi na vile vile barua za kimapenzi alizozipokea kutoka kwa Morini na kuzituma kwenye kituo kimoja cha televisheni. Padre Morini alijulikana kwenye paroko yake kama "Padre Euro" kwa sababu ya alivyowasisitizia waumini kumpa pesa.

Mwingine ambaye pia anapelelezwa ni Askofu Giovanni Santucci wa Massa Carrara, ambaye aliilazimisha kampuni moja ya bima ya Kikatoliki kuongeza alama za ulemavu wa Padre huyo.

#newsPmbjxwqsei