sw.news
65

L'Espresso Huanza Upya Shutuma dhidi ya Kadinali Rodriguez

Yule pro-Francis L'Espresso (mwezi wa Februari tarehe tano) atasimama na shutuma dhidi ya Kadinali Óscar Rodriguez Maradiaga wa Tegucigalpa, Honduras.

Desemba, gazeti la Uitalia ulishutumu Rodriguez kwa kupokea kila mwaka euro 500,000 kutoka kwa Chuo Kikuu cha Ukatoliki cha Tegucigalpa na kuharibu Dola milioni 1.2 kupitia uwekezaji zisizofaa kule London.

Rodriguez alijibu kuwa malipo hayakunuiwa kuwa yake kibinafsi bali ya miradi ya kiuchungaji.

Lakini L'Espresso anaonyesha kuwa malipo yalienda kwa akaunti yake ya kibinafsi, na si kwa mojawapo ya dayosisi kuu. Msaidizi wa Askofu Rodriguez Juan Posé Pineda pia alipokea pesa.

L'Espresso anaonyesha kuwa fedha nyingi hazikunukuliwa kwa mizania ambayo Rodriguez aliwasilisha mwezi wa Septemba 2017 kwa Vatikani wakati wa Kuzuru Ad-Limina. Mizania hio haionyeshi ushahidi ya zaidi ya euro milioni moja ambayo askofu msaidizi Pineda aliyopokea kutoka kwa serikali.

Madai mengine yanatoka kwa Martha Alegria Reichmann, mjane wa Alejandro Valladares, balozi wa zamani wa Honduras kwa Holy See kwa miaka ishirini na miwili. Rodriguez ambaye alikuwa rafiki ya familia ile, aliwasadikisha kuwekeza akiba zao na mfadhili wa London Youssry Henien, Henien huyu yuyu ndiye aliyefanya Rodriguez kupoteza euro milioni 1.2 ya dayosisi yake kuu. Reichmann alitambua mwezini wa Februari 2015 kuwa pesa zilikuwa zimepotea. Majaribio ya kumpigia Henien au Rodriguez hayakufua dafu.

Kufikia sasa Rodriguez alijitetea kwa kusema kuwa upinzani dhidi yake ulikuwa shambulio dhidi ya "mageuzi "ya Papa Francis.

Picha: Oscar Rodríguez Maradiaga, © Gabriele Merk, CC BY-SA, #newsGcxvcfmjhm