sw.news
51

Cardinal Müller, "Sielewi Mbona Hakuna Mazungumzo

Katika mahojiano na Il Foglio kinara wa Shirika la Mafundisho ya Imani aliyefutwa kazi, Kadinali Gerhard Ludwig Müller anasisitiza kuwa amekuwa mwaaminifu kwake Papa Francis, "Kamwe hili halikua suala la uaminifu kafanywa sifa tupu."

Alipoulizwa kumhusu Kadinali mtetezi ushoga wa Vienna Christoph Schönborn ambaye alisema kuwa msimamo wake kuhusiana na Amoris Laetitia huhitilafiana na msimamo wa Müller, alijibu, "Huenda ikawa kuwa ni Kadinali Schönborn ndiye aliye na maono tofauti na yangu, lakini huenda maono yake yakapinga maono aliyokuwa nayo hapo awali kabla yake kubadilisha fikra zake."

Kusuhu mkatao wa Papa Francis kuwa na mazungumzo na Makadinali wa Dubia Müller alisema, "Sielewi mbona hakuna mazungumzo tulivu." Aliongeza kuwa, " Hadi wa leo, cha pekee nilichokiskia ni kemeo dhidi ya Makadinali hawa. Lakini hii sio njia wala sio sauti mwafaka ya kusonga mbele." Na " Sisi Maaskofu tunayo haki, ningesema, haki takatifu kujadili wazi wazi."

Bila kutaja jina lolote, Kadinali Müller anakosoa tamanio la PapaFrancis kwa mazingira, "Tunao walei wengi ambao ni wataalam wa masuala hayo", alisema, "Yesu hakuwapa Mitume jukumu juu ya serikali ya kidunia. Viongozi maaskofu waliishi karne zilizopita, na hawakuwa wazuri kwa Kanisa."

Picha: © Jeon Han, korea.net, CC BY-SA, #newsKlbprcwukm