sw.news
52

Papa Francis Hajakaribishwa Nchini Argentina

Wasemaji wa Papa Francis wa mrengo wa kushoto nchini Argentina ambao huibua na kusababisha kashfa za kisiasa, ndio sababu ya uwezekano wa Francis kukumbwa na upinzani mkuu wakati wa ziara yake katika nchi alikozaliwa.

Mmoja wa wachochezi hao wa Francis ni Juan Grabois (34), mwanawe kiongozi wa kihistoria wa Kiperoni na mwanaharakati wa mrengo wa kushoto. Kulingana na Sandro Magister yeye ni "rafiki wa karibu wa Bergoglio hivi kwamba unawezakudhania kuwa kila ya maneno yake hueleza dhana halisi za kisiasa za Papa Francis."

Francis alimteua Grabois kuwa mshauri wa Baraza la Upapa la Haki na Amani. Nchini Argentina, maneno yake chochezi dhidi ya serikali ya Marci huhusishwa na Bergoglio.

Kwa ajili ya ziara ya Francis nchini Chile Grabois aliandaa safari ya wafuasi 500 wa mrengo wa kushoto amabao wataketi katika mstari wa mbele katika ibada ya misa ambayo itaongozwa na Papa Francis mnamo tarehe 17 mwezi Januari mjini Temuco, nchini Chile. Badaa ya ibada hiyo, Francis atashiriki chakula cha mchana na baadhi yao.

#newsXnojhvpybt