sw.news
78

Müller: "Kamwe Sitampinga Papa Francis"

Kadinali Gerhard Müller hakubaliani na "vikundi vya kitamaduni" ambavyo kulingana naye vingetaka kumwona akiongoza kikundi dhidi ya Papa, " Kamqe sitafanya hivyo".

Müller aliambia corriere.it (Novemba 26) huwa hamkubalishi yeyote kutumia "mabaya yaliyomkabili hapo awali katika miezi kadhaa iliyopita" kwani kama Kadinali yeye "kwa njia asili huwa pamoja na Papa".

Müller alijibu kuwa kuna "mizungu" iliyomzingira Francis na ambayo hujihusisha na "kuwapeleleza wanodaiwa kuwa maadui" na kuwaainisha watu kama marafiki zake Francis au maadui. Francis alimwambia Müller kuwa alishutumiwa kwa kuwa "adui" jambo ambalo kulingana na Müller ni "lisilo na msingi" .

Müller anaamininkuwa taharuki iliyoko Kanisani ni kati ya "kikundi kikali cha kitamaduni katika baadhi ya mitandao na kwa kiwango sawa kikundi cha kistaarabu kilichotiliwa chumvi".

Picha: © michael_swan, CC BY-ND, #newsMxgwlkiupk