sw.news
45

Wanachoweza Kukisoma Wakatoliki Kutoka Kwa Papa Mhuria Francis - Na Padre Reto Nay

Baada ya Kardinali Müller kuachishwa kazi, kuna utata iwapo Papa Francis ni Papa wa Wahuria wakali tu. Ni Papa Wa Kardinali Kasper, Cupich, and Coccopalmerio.Si Papa wa Kardinali Müller, Burke au Caffarra. Francis sio Papa wa Wakatoliki.

Tofauti kati ya Francis ambaye ni mhuria na mtangulizi wake ambaye ni mhifidhina inaweza kubainika kwa kuzingatia mateuzi yao. Makisio yangu ni kuwa, kati ya mateuzi kumi muhimu yaliyofanywa na Papa JohnPaul II au Benedict XVI nane yalikuwa ya kihuria, mawili yalikuwa ya kihifidhina. Chini ya uongozi wa Papa Francis, kati ya mateuzi kumi, kumi ni ya kihuria.

Kutokana na hili tunaweza kupata mambo mawili. Kwanza ni lazima, tulifurahie azimio la Francis katika kuendeleza ajenda yake ya kihuria na kuwaangamiza anaowachukuwa kuwa maadui zake.Tafakari kuwa, hivi maajuzi kungekuwa na Papa aliye na maazimio sawa kuyakweza mabo yote memea na chochote kilicho cha Kikatoliki.

Pili, ni lazima tuelewe kuwa ufufuo wa Kanisa hautatokana na wahuria wala wahifidhina. Francis huskuma mbele ajenda za kihuria ambazo tayari tunajua zimekosa kufaulu, tangu kutekelezwa katika mataifa mengi, hata kabla ya Francis kuwa Papa. Katika nchi hizi zote, sasa Kanisa lin abomoka. Ufufuo hautatokana na wafhifidhina, kwani wao ni aina ya wahuria wenye tofauti ndogo sana

Ufufuo huo utaletwa na Wakatoliki walio na imani, kwanza, katika Liturgia ya Kikatoliki, na kama matokeo, katika Imani ya Katoliki. Kutoka kwa Familia za Wakatoliki hawa, kizazi kipya cha wachungaji, uongozi mpya, utazaliwa.

Picha: © Greater Boston Tridentine, CC BY-NC, #newsYosiakmdyy