sw.news
42

Afisa Wa Polisi Aliyeuawa Alikuwa Amebadili Dini Na Kuwa Mkatoliki

Usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi (Machi 23/24), Arnaud Beltrame, 45, afisa wa polisi Mfaransa mwenye cheo cha luteni kanali, aliaga dunia kutokana na majeraha ambayo aliyapata wakati wa oparesheni dhidi ya magaidi.

Alikua amejitoa kama mateka kwa kuchukua nafasi ya mwanamke ambaye alikuwa ameshikwa na gaidi Radouane Lakdim kama mateka wa mwisho katika duka la Super U huko Trebes.

Beltrame alikuwa na matumaini ya kujadiliana na Lakdim baada ya wanunuzi hamsini na wafanyikazi ambao walijikuta kwenye shambulizi hilo kupelekwa pahali salama.

Lakini Lakdim, ambaye alikiri utiifu wake kwa Islamic State, alimpiga risasi na kumdunga, jambo lililowafanya polisi kushambulia na kumwua mshambulizi huyo.

Tayari Betrame alikuwa amekamilisha masaa 30 ya matayarisho ya ndoa yake ya kidini na Marielle, daktari wa wanyama, ambaye walikuwa wakiishi pamoja katika ndoa ya kimila bila watoto. Sherehe hiyo ilikuwa imeratibiwa kufanyika mwezi Juni.

Alipokea desturi zake za mwisho za dini kutoka kwa Padre Jean-Baptiste wa makao ya watawa ya ibada ya kale ya Chanons of Lagrasse. Wapenzi hao walikutana naye mnamo mwaka wa 2016 wakati wa ziara kwenye makao hayo ya watawa.

#newsSkyarwvkse