sw.news
70

Udanganyifu Wa Papa Francis Wafichuliwa

Papa Francis amedhibitisha kuwa Askofu Marcelo Sánchez Sorondo ndiye Chansela wa Chuo cha Upapa cha Sayansi, ingawaje yeye ana umri uliozidi miaka 75 na ameshikilia wadhfa huo tangu mwaka wa 1998. Sánchez ni mwenye itikadi kali za hali linganifu.

Mnamo mwezia Juni Francis alimsimamisha kazi Kadinali Müller kama Kinara wa Shirika la Mafundisho ya Imani kwa kisingizio kuwa hakutaka kuendeleza mamlaka katika uongozi wa Vatikani muda zaidi ya miaka mitano.

Hili limekuja kuwa uwongo mtupu. Viongozi wengine wahuria kama vile Kadinali Tauran, Kadinali Ravasi au Mkuu wa tume ya Roman Rota, Monsignor Pinto, tayari wametimiza vipindi vyao vya miaka mitano ila Francis bado amewaachia majukumu.

Picha: Marcelo Sánchez Sorondo, © Gcmarino, wikicommons CC BY-SA, #newsHkuwzhjppk