sw.news
64

Shuke Ya Nyakati Zijazo; Shule Ambapo Somo La Kilatini Ni La Lazima

Shule ya Kikatoliki ya Mission Dolores iliyoko mjini San Francisco, shule ya nyakati zijazo, ina watoto kutoka malezi ya Kiingereza, Kihispania, Kitagalog na Kieritria. Katika Kilatini wao hupata usawa na lugha ya kuwaunganisha ambapo hakuna mwanafubzi aliye baguliwa dhidi ya kukuza uwezo wa lugha. Hivyo basi somo la Kilatini ni la lazima kwa wanafunzi wa chekechea hadi daraja la nane.

Programu hiyo ilizinduliwa katika mwaka huu wa masomo. Utafiti umeonyesha kuwa somo la Kilatini huchangia ghafla katika ukuaji wa msamiati wa mwanafunzi na vile vile uwezo wa kusoma ufahamu. Pia huchangia katika kufanya vyema katika masomo ya Sayansi.

Somo la Kilatini hufunzwa katika viwango vitatu, huku kila kiwango kikifunzwa kwa vipindi viwili kila juma. wanafunzi wa chekechea na wa daraja la kwanza na daraja la pili huwa na kipindi cha dakika 20; wale wa daraja la tatu kufikia la tano huwa na kipindi cha muda wa dakika 30-40 na wale daraja la sita hadi daraja la nane huwa na kipindi cha lisaa limoja.

Picha: Mission Dolores Academy, © Samantha Alfonso, #newsDnehfsbryk