sw.news
66

"Iweje Vatikani Inashiriki Katika Mazungumzo Ya Maridhiano Ilhali Uchina Inaendelea Kubomoa Makanisa?"

Mnamo tarehe 29 mwezi Agosti maafisa wa usalama walijaribu bila sababu yoyote kubomoa kanisa la Kikatoliki lililo Wangcun, katika Dayosisi ya Changzhi. Kwa wakati mmoja takriban makasisi ishirini pamoja na waumini 2000 waliungana ili kuzuia tinga tinga hizo. Makasisi kadhaa na walei walidhulumiwa, mmoja kutandikwa na kujeruhiwa kichwani na afisa mmoja wa polisi. Wafanyakazi hao walishindwa kuendeleza juhudi zao.

Tukio hili ni mojawapo tu ya ubomoaji wa makanisa mengi ya Kikatoliki nchini Uchina katika nyakati za hivi maajuzi. Padre Alexander Lucie-Smith aliuliza kwenye Catholic Herald, “Iweje Vatikani Inashiriki Katika Mazungumzo Ya Maridhiano Ilhali Uchina Inaendelea Kubomoa Makanisa?"

#newsBeirckneec

02:02