sw.news
67

Maafikiano Ya Kisiri Ya Kardinali Schonborn na Mashoga wa Vienna

Gazeti la Kidayosisi la Dayosisi Kuu la Vienna "Sonntag" limemsifu Gery Keszler (53), mwanaharakati wa ushoga mwenye virusi vya ukimwi na mwanzilishi wa shirika la Vienna "Life Ball" moja ya sherehe kuu ya Mashoga Uropa ambalo wakosoaji huliita "Death Ball"

Keszler analiambia gazeti hilo kuwa angekuwa mwenye furaha kumkaribisha Kardinali wa Vienna Christoph Schonborn (72) kwenye sherehe ya mwaka huu mnamo Juni 10. Kulingana naye, " Shirika la Life Ball na Kanisa wana malengo sawa," Yeye ni rafiki wa karibu sana wa Schonoborn. Wao hupatana kisisrisiri kushiriki chajio pamoja.

Ni miaka mitatu tu iliyopita ambapo Schonborn alieleza shirika hilo tatanishi la "Life Ball" kama "La kuhuzunisha" huku akisema kuwa: "Kweli tunahitaji haya, Sherehe hii la kipagani? Je, kweli hii ndio yenye kuleta furaha? Ama si ni heri tuseme kuwa tunawaonea huruma watu ambao hushiriki kwenye sherehe kama hii."

Picha: Christoph Schönborn, © Cornelius Inama, CC BY-NC-ND, #newsWqusjljwvi