sw.news
47

Mshangao: Vatikani Ilimkataza Mwanasiasa Mtetezi Ushoga Kuzungumza

Aliyekuwa rais wa Ayalandi Mary McAleese hakupatiwa nafasi ya kuzungumza katka mutano wa wanawake mnamo tarehe 8 mwezi Machi huko Vatikani. Tarehe 8 mwezi Machi ilifanywa "Siku ya Kimataifa ya Wanawake" haswa na shirika la kisoshalisti na mataifa ya kikomunisti.

Kulingana na kituo cha Irish Independent (Februari 2), Kadinali mzawa wa Dublin Kevin Farrell hakukubalisha hotuba ya McAleese na ya wazungumzaji wengine wawili kwa sababu ya nafasi zao za kuunga mkono ushoga. Suluhu la Kifarisayo lilipatikana kwa haraka: Waandalizi waliupeleka mkutano huo mahali pengine, ukumbi wa makao makuu ya Wayesu yaliyo Roma.

Hivi maajuzi McAleese alidai kuwa mwanawe ambaye ni shoga, Justin alipitia "mateso" kwani hangeyavumilia mafunzo ya Kikatoliki kuhusiana na ushoga. Hivi maajuzi, Vatikani imekuwa ikiwaalika wazungumzaji watetezi ushoga na watetezi wa uavyaji mimba.

Picha: Mary McAleese, #newsOrmfbipjum