sw.news
53

Mpinzani Wake Kadinali Pell Afariki

Damian Dignan, mpinzani wa Kadinali George Pell, alifariki mnamo siku ya Jumamosi mjini Balllarat, nchini Australia, kutokana na Lukemia. Alikuwa mmoja wa wanaume watatu waliokumbwa na utata ambao walimkashifu Kadinali George kwa "kuwashika sehemu zao nyeti" kwenye kidimba cha kuogelea mnamo mwaka wa 1972.

Dignan alikuwa na historia ya kuzua vurugu na aliwahi kutiwa mbaroni kwa uendeshaji gari angali mlevi. Pia aliwahi kuwakashifu walimu wake. Mkewe msimamizi wa kidimbwi hicho cha kuogelea alitoa ushahidi kuwa " yeye wala mumewe hawakushuhudia chochote cha kushukiwa".

Pell atakuwa na kikao mnamo mwezi Machi kitakacho toa uamuzi iwapo atakabiliwa na hukumu halisi ya majaji. Amezidi kuyakana mashtaka hayo.

#newsVqvqhjngen