sw.news
77

Mwanaume Anayefunga Ndoa Na Talakilishi Mpakato Ashtaki Serikali Akitaka Kutambulika

"Dereva" aliyejitambulisha Chris Sevier amesema kuwa alifunga ndoa na talakilishi yake mjini New-Mexico, nchini Marekani. Kisha alimshtaki mwokaji mmoja aliyekataa kumwokea Keki ya harusi yake na talakilishi yake "talakilishi bi. Harusi", kulingana na taarifa za Washington Post. Mwokaji huyo huyo pia alikuwa ameshtakiwa tena kwa ajili ya kukataa kuoka keki ya ndoa ya kishoga.

Sevier anataka kuwa na haki sawa kama shoga kwa ndoa yake isiyo ya kitamaduni. Pia alilishtaki jimbo la Utah akitaka "ndoa" yake Kutambulika. Hakimu mmoja amekubalisha sehemu za mashtaka hayo kuendelea.

Picha: © Jeremy Brooks, CC BY-NC, #newsYmdcnwncia