sw.news
51

Kifo Cha Kasisi Kijana Bado Kinashangaza

Uchunguzi wa maiti haujafanikiwa kubainisha kilichosababisha kifo cha padre Mhindi Martin Xavier Vazhachira (+33), ambaye alitoweka kwa hali ya kutatanisha kutoka Edinburgh, Scotland, vyombo vya habari vya Scotland vimetangaza. Alipatikana akiwa amefariki katika ufuo wa Edinburgh, Scotland, mnamo Juni tarehe 24, takriban kilomita 40 kutoka nyumbani mwake, baada ya kutokweka kwa muda wa siku nne. Vazhachira aliyekuwa wa shirika la Wakarmeli wa Bikira Maria, aliwasili Scotland mnamo Oktoba mwaka wa 2016. Alifanya kazi katika kanisa la St John the Baptist, corstorphine na alikuwa akimaliza masomo yake ya shahada ya uzamifu katika Cuo Kikuu cha Edinburgh.

#newsCmkrwsxwkx