sw.news
40

Tuzo La Jacques-Hamel Hukweza "Mazungumzo Kati Ya Dini Tofauti" Na Waliokuwa Wakatoliki

Tuzo la Jacque-Hamel-Price awamu ya 2018, lililobuniwa na Muungano wa Vyombo vya Habari nchini Ufaransa (Federation of Catholic Media), liliandaliwa mnamo tarehe 26 mwezi Januari na kumwendea mwanahabari Samuel Lieven wa La Croix kwa ajili ya nakala yake “Thomas na Benoît, waongofu wa Novemba 13” (Thomas et Benoît, les convertis du 13 novembre).

Tuzo hilo huitwa kwa jina lake Padre Jacques Hamel ambaye aliuawa mjini Saint-Étienne-du-Rouvray, nchini Ufaransa, mnamo mwezi Julai mwaka wa 2016 wakati wa Ibada Takatifu.

Nakala hiyo yake Lieven inasherehekea "ubadilishaji dini" wa Thomas ambaye ni mzawa wa familia yenye msingi dhabiti wa Kikatoliki, mamake ni mwalimu wa dini, lakini aliiasi imani yake na kuwa Mwislamu dhabiti. Sasa yeye hulea ndevu, mkewe Lila pia ni mwongofu, huvalia buibui na wana watoto watatu: Abdallah, Amin na Issa. Thomas alifungua maktaba ya Kiislamu ambayo polisi walichunguza baada ya shambulizi la kigaidi huko Bataclan, nchini Ufaransa.

Baada ya muda mrefu Thomas alirejea kwa Familia yake, haswa kakaye Benoît,, aliyekuwa mwanaseminari na rafiki wa karibu wa Jamii ya Franciscan Friars of the Renewal.

Ni kana kwamba Tuzo hilo la Jacques-Hamel linalenga kukweza aona hii ya "mazungumzo kati ya dini tofauti". Tuzo hilo liliwasilishwa mjini Lourdes na Kadinali Pietro Parolin, Waziri wa Vatikani wa Masuala ya Nchi za Kigeni.

Picha: la-croix.com, #newsBmoqnyonsf