sw.news
19

Gloria.tv: Kama Mnavyoona, Malengo Yetu Yako Juu

Tangu msimu wa kiangazi uliopita Gloria.tv imeongeza idadi ya watumizi wake. Hivi sasa sisi huchapisha habari katika lugha kadhaa. Hili husababisha msongo kwenye sava zetu. Mnamo mwaka wa 2017 hatukua na budi ila kulipa zaidi ya dola 30, 000 kugharamia kompyuta za sava, ufuasi na stima katika vituo kadhaa vya data. Hizi ni pesa nyingi kwetu - lakini chache ikilinganishwa na kiasi cha uhubiri wa Gloria.tv.

Gloria.tv imeendelea kukua licha ya mikakati amilifu kwenye mitandao ya kijamii na mitandao ya kutafuta kubagua dhidi ya maudhui ya Kikatoliki na yale ya kihifidhina. Tuliona hili tangu msimu wa kiangazi uliopita - muda mrefu kabla ya vyombo vya habari kuanza kuzungumza kuhusu jitihada hizi - kwamba tulikuwa tukipoteza wafuasi kutoka kwao. Lakini tumeweza kufidia na kukua.

Kiasi kikubwa cha fedha zetu hutokana na barua za uchangishaji wa pesa. Tunatumaini na kuomba kwamba kupitia kwa kampeni hii ya mtandaoni ya msimu huu wa Kwaresima tutapokea dola 10,000 zaidi. Kufikia sasa tumeweza kupata takriban dola 4,000.

Gloria.tv hutegemea neema na ukarimu wako. ni changamoto kuu kudumisha kazi yetu ambayo inaendelea kupanuka. Msaada wako huwezesha Gloria.tv. Tusaidie kutimiza lengo letu la kampeni hii la dola 10,000 kufikia Pasaka, tafadhali.

Tafadhali, jiunge na kampeni ya msimu huu wa Kwaresima ya Gloria.tv

#newsCaixdcgzei