sw.news
25

Askofu Mkuu Wa Guam Apatikana Na Makosa Ya Dhulma Za Kishoga

Tume ya majaji watano wa Vatikani wamempata Askofu Mkuu Anthony Apuron na makosa ya kuwadhulumu kishoga vijana wa kiume miongo iliyopita. Tume hiyo ilitangaza uamuzi wake katika ujumbe kwa wanahabari (Machi 16).

Apuron "alipatikana na baadhi ya makosa aliyodaiwa kuyafanya". Ataadhibiwa kwa kung'atuliwa afisini na kupigwa marufuku dhidi ya kuishi kwenye kisiwa cha Guam.

Jaji aliyekuwa akiyaongoza mashtaka hayo alikuwa Kadinali Raymond Burke, mtaalam katika sheria ya Kanisa.

#newsHhmmpedogd