sw.news
70

Kardinali Müller, "Hakuna Mgogoro Kati Yangu Na Papa"

Papa Francis alimfahamisha Kardinali Gerhard Müller (69) mnamo siku ya Ijumaa, kuwa angeng'atuliwa kutoka kwenye nafasi yake kama kinara wa Shirika la Mafundisho ya Imani siku moja baadaye.

Müller aliambia jarida la Ujerumani la "Allgemeine Zeitung" kuwa alishangazwa na uamuzi huo, lakini hakushtuka, "Hakuna mgogoro kati yangu na Papa Francis." Francis alimwambia Müller kuwa kwa jumla hatazidisha mihula hiyo ya miaka mitano, na kuwa Müller atakuwa wa "kwanza" kuathiriwa na mabadiliko haya.

Müller "hababaishwi" na kuachishwa kazi, "Ni lazima kila mtu astaafu wakati mmoja." Atabaki Roma na na kuendeleza miradi ka Kichungaji na ya Kisayansi. Hata hivyo Müller anajuta, kuwa majumaa kadhaa yaliyopita Francis aliwafuta kazi watatu wa "wafanyikazi wake bora ." Kulingana na ripoti ya vyombo vya habari walikuwa wamedhubutu kumkosoa Francis.

Picha: © Piotr Drabik, CC BY, #newsXfyscrkosi