sw.news
64

Shule Za Kikatoliki Zaondoa Sanamu 162 Ili Kuwaunganisha Wengi

Shule ya msingi ya Kikatoliki ya San Dominico iliyo San Anselmo, katika jimbo la California, iliondoa sanamu zake zote ila 18 ya sanamu 180 na michoro takatifu kutoka kwenye chuo hicho, kulingana na ripoti za marinij.com kwa sababu inayoemekana kuwa shule hiyo inapania kuwa "unganifu zaidi". Shule hiyo ilianzishwa mnamo mwaka wa 1850 na huwahudumia wanafunzi 671.

Sanamu kubwa ambayo iliondolewa, ni Bikra Maria kamshika Mwanawe Yesu mikononi mwake. Sanamu hiyo ilikuwa katikati mwa behewa la shule hiyo na wakati wa sherehe maalum wanafunzi waliirembesha sanamu hiyo. Hivi sasa sanamu hiyo imo kwenye lelo.

Miaka kadhaa iliyopita Shule ya San Domenico iliondoa jina "Catholic" kutoka kwenye kauli ya kazi ya shule hiyo. baadaye waliacha kuwatayarisha wanafunzi kwa maungamo na Ekaristi ya kwanza. Hatimaye nembo ya shule hiyo pia ilibadilishwa.

#newsDvbizhkvta