sw.news
73

Mwanachama Wa Opus Dei Akweza Itikadi Za Kishoga

Meya wa Las Condes, nchini Chile, Joaquín Lavín anaunga mkono kukubalika kwa ushoga. Alipokuwa kwenye kituo kimoja cha Televisheni cha Chile Chilevisiónalisema kuwa "Masuala hayo yanastahili kujadiliwa." Lavín alihadithia tukio la binti ya mraibu wa madawa ya kulevya katika manisoaa yake, ambaye anasemekana kulelewa na shoga wawili. Kulingana na Lavín ni heri msichana huyo anavyoishi na shoga hao badala ya kuwa na familia yake. Hata alidai kuwa sasa msichana huyo "ni mwenye furaha".

Lavín ambaye ni baba ya watoto saba, ni mwanachama maarufu wa Opus Dei. Alijaribu mara mbili kugombea kiti cha urais cha Chile.

Mnamo tarehe 18 mwezi wa Mei aliweka bendara katika ofisi yake ya manispaa ili kuadimisha sikukuu ya "utofauti wa kijinsia". Lavín alieleza kwenye mtandao wa Twitter, kuwa bendera hii ilikuwa " ishara ya heshima na kutobagua".

Picha: Joaquín Lavín, © Sebastián Piñera E., CC BY-SA, #newsBuictnunms