sw.news
63

Ujerumani Yaanzisha Desturi Ya Ndoa Ya Wake Wengi

Mahakama kuu ya Ujerumani, Verwaltungsgerichtshof, iliamua kuwa, Mwislamu Msiria, mwenye umri wa miaka 36, aliye na wake wawili, ataregeshewa paspoti yake.

Mnamo mwaka wa 2008 Msiria huyo alimwoa mwanamke Mjerumani mjini Karlsruhe, na majuma saba baadaye akamwoa binamu yake kutoka Siria. Miaka miwili baadaye alipokea uraia wa Ujerumani. Baada ya ndoa yake na wake wawili kujulikana alinyang'anywa uraia wake kwani alimwoa mke wake wa pili, alipokuwa akipatiwa uraia wa Ujerumani.

Uamuzi wa mahakama ambao ulishikilia uamuzi huu sasa umebatilishwa. Wake wote wawili huishi Karlsruhe lakini katika nyumba tofauti.

Picha: jungefreiheit.de, #newsFpvolsfrap