sw.news
97

Franciz Afutilia Mbali "Taasisi Ya Ndoa Na Familia"

Taasisi Ya Upapa ya Ndoa na Familia, ya Roma, iliyoanzishwa na John Paul II kulinda kutoangamizwa kwa ndoa za Kikristo na kupigana na uavyaji, imefutiliwa mbali katika hali yake ya sasa na Papa Francis kupitia kwa barua yake ya hivi maajuzi al maarufu motu propio. Taasisi hiyo sasa itakuwa ikiitwa "John Paul II Pontifical Theological Institute for Marriage and Family Sciences". Taasisi hiyo ilikumbwa na adhabu ya Francis kwa sababu ya ilivyolinda mafundisho ya Kikatoliki wakati wa Sinodi la Familia, ingawaje Francis aliitenga taasisi hiyo na kazi za Sinodi hilo.

Sasa, Francis angetaka taasisi hiyo ieneze nakala yake tatanishi ya Amoris Laetitia ambayo hupuuza kutoangamizwa kwa ndoa za Kikristo. Pia jambo hili limechukuliwa kama pigo kuu dhidi ya John Paul II.

Kulingana na mpango usioeleweka vyema, motu propio haswa inafutilia mbali mafundisho ya Kikatoliki na kazi ya uchungaji kama "utaratibu na mifumo ya kale", kisingizio cha kawaida cha kutupilia mbali nafasi ya wapinzani bila kutoa hoja zozote.

Motu Propio iliyotolewa mnamo tarehe 19 mwezi Septemba, imeandikwa tarehe 8 mwezi Septemba. Hii ni siku mbili baada ya kifo cha Kadinali wa Dubia Carlo Caffara, rais mwanzilishi wa taasisi hiyo, ambaye alikuwa mkosoaji mkali wa Amoris Laetitia.

Kwa kuchukua hatua hii, Francis anazidisha utengano katika Kanisa Katoliki.

#newsXzzkidcyff