sw.news
79

Baba Mtakatifu, Msaidie Charlie

Kundi la kina baba na kina mama kutoka Roma limetuma ombi kwa Papa Francis, Askofu wa Roma, kusaidia katika kumwokoa Charlie Gard, mtoto mzungu mwenye umri wa miezi tisa, anayeugua kutokana na ugonjwa nadra wa kijenetikia na ambaye mahakama ya Uropa ya Haki za Kibinadamu inataka afe dhidi ya mapenzi ya wazazi wake.

"Twaja mbele zako kama watoto, wanaomwandikia baba yao", ombi hilo linasema.

"Twaja kwako wewe kama baba, na kukuomba: ni lipi utakalo tulifanye, sisi wana wako, raia wa dunia, wa Uropa, wa Italia? Tuambie, tusaidie, tufariji. Usituache mashakani. Twangoja kupokea ishara kutoka kwako, ili tusihisi upweke katika mapambano haya ya maombi ambayo tumeyaanzisha kwa ajili ya Charlie.

Twakupenda kutoka kwenye kina cha nyoyo zetu kama tumpendavyo Charlie, kwani hakuna, moyo ulio wa maana zaidi kushinda moyo mwingine. Charlie amekuwa mwana wetu sisi wote, na wako pia.

Twangoja kwa imani."

Barua hiyo imepigwa sahihi na Gemma na Federico Piro na Maria Elena na Giuseppe Fiacco.

Ili kushiriki kwenye ombi hilo, tuma kwa alpapaxcharlie@gmail.com

Picha: Charlie Gard, facebook, #newsPbitsdpmtr