sw.news
66

Papa Francis "Huongozwa" Na "Mafunzo Ya Ubudha"

Papa Francis aliwasifu Budha na Mtakatifu Francis wa Assisi ila akampuuza Kristu alipokuwa akiwahutubia Watawa wa Ubudha manmo tarehe 29 mwezi Novemba huko Yangon wakati wa safari yake ya uchungaji huko Myanmar.

Francis alieleza "heshima yake kwa wote walioko Myanmar ambao huishi kulingana na tamaduni za kidini za Ubudha". Aliongeza, "Kupitia kwa mafunzo ya Ubudha, na ushahidi maalum wa watawa wengi, watu wa humu wamekua katika misingi ya subira, uvumilivu ma heshima kwa maisha."

Francis ana imani kuwa maneno ya Budha hutoa "mwongozo kwa kila mmoja wetu" "kukabiliana na hasira kwa kutokasirika" na "waovu kwa wema".

#newsUhqmdsxxom