sw.news
63

Rabbi, " Mahali Popote Ambapo Ukristu Unadidimia, Upagani Unakita Mizizi"

Rabbi Elad Dokow, mwalimu katika Taasisi ya Israeli ya Technion Institute of Technology alitoa maoni yake kuhusiana na sanamu ya mungu wa Kigriki Pallas Athena ambayo ni sehemu ya maonyeshiokatika makao makuu ya shirika la U.N mjini New York kwa udhamini wa Falme za Kiarabu almaarufu United Arab Emirates.

Akizungumza na Breaking Israel News alihusisha sanamu hiyo na "chipuko la upagani na uabudu wa miungu duniani". Alieleza kuwa upagani humkubalisha mtu "kubuni ukweli wake" na Umoja wa Mataifa (U.N) ni kama Upagani "mahala pa ukweli bandia uliobuniwa kwa kura".

Dokow alitamatisha, " tunachokishuhudia leo hii ni kuwa mahali popote ambapo Ukristu unadidimia, upagani na uabudu wa miungu unakita mizizi, na unakotoweka Ukristu, mambo ya kutamausha hutendeka."

Picha: © Giacomo Brings, CC BY-NC, #newsCwxxikyfbe