sw.news
11

"Ushambulizi Wa Francis Dhidi Ya Useja Hufuata Ratiba Fulani"

Papa Francis anataka kulibadilisha Kanisa kwa mchakato wa polepole ili kuzuia utengano ambao unaeza kutokana na mbinu ya kustua na kuhofisha, kulingana na mwanahabari Mjerumani Müller-Meiningen.

Akiandika kwenye mtandao wa zeit.de (Machi 9), alieleza kuwa Francis ni "mjuzi mwenye busara" ambaye tayari aliingiza Ekaristi kwa wazini na analenga "kushambulia useja", "Matayarisho ya kutekeleza hili hayajafichwa kamwe, ila yanafuata ratiba thabiti."

Mjadala wa kwanza dhidi ya useja utakuwa wakati wa Sinodi la Vijana linalokuja mnamo mwezi Oktoba mwaka wa 2018 a kisha mjadala mkuu utakuwa katika Sinodi la Amazon. mnamo mwaka wa 2019.

Kulingana na Müller-Meiningen, "kitimbi" cha Francis kinahusisha kufutilia mbali tabia kwa kuzipuuza katika "kesi binafsi". Hili linaweza kutumika pia kwa shoga, upangaji uzazi bandia na mashemasi wa kike.

Picha: © Mazur, thepapalvisit.org.uk, CC BY-NC, #newsQgadmsyohs