sw.news
68

"Wakati Wowote Mapadre Wakikutana, Wao Huzungumzia Jinsi Bergoglio Alivyo Mbaya"

Papa Francis ana umaarufu mwingi kati ya watu walio mbali kidogo na Kanisa, kulingana na ripoti za gazeti lipingalo Kanisa la The Guardian (Oktoba 27). Kanisani kuna "chuki na uoga".

Gazeti hilo la mrengo wa kushoto lilimnukuu kasisi maarufu Mwingereza akisema: "Tunasubiri kwa hamu kifo chake [Francis]. Tukisemacho faraghani hakiwezi kuchapishwa. Wakati wowote Makasisi wawili wakutanapo, wao huzungumzia jinsi alivyo mbaya Bergoglio... Yeye ni kama Caligula: angekuwa na farasi, angemteuwa awe kadinali."

Akieleza matokeo ya ukandamizaji ambao Francis anausambaza Kanisani, Kasisi huyo alizidi kusema: "Kamwe msichapishe chochote nilichokisema, au nitafutwa kazi."

Picha: © korea.net, CC BY-SA, #newsInfifmclaa