sw.news
53

Mkuu Wa Shirika La Agostino, "Madhara Yaliyosababishwa Na martin Luther Yalikuwa Makuu"

Martin Luther alisababisha mpasuko wa Ukristo katika Mataifa ya Magharibi na kuunda misingi ya mambo ya kilimwengu na uenezaji wa itikadi za kilimwengu, Mkuu wa shirika la Agoatino Padre Alejandro Moral Antón aliandika kwenye barua kwa shirika lake (Septemba 28). Luther mwenyewe alikua Mwagostino.

Padre Moral anaongeza kuwa "Bali na kuachana na shirika hilo, Luther alichukia maisha ya kidini kadri ya uwezo wake, akatupilia mbali tamaduni za kujinyima pamoja na ucha Mungu, akatupilia mbali maombi ya "breviary" pamoja na majukumu mengine, akabadilisha teolojia ya Sakramenti vikali, akakashifu kiapo na kukweza kuondoka kwa wanadini waliokula kiapo."

Na,"Madhara yaliyolikumba shirika hilo na maisha ya Kidini nchini Ujerumani yalikuwa makuu."

Picha: Luther in Hell, by Egbert II van Heemskerck, #newsUkfldsdjvh