sw.news
56

Je, Francis Anataka Maadili Ya Matajiri? Na Padre Reto Nay

Mtandao wa Maaskofu wa Ujerumani katholisch.de ulieleza mnamo tarehe 20 mwezi Septemba, kuwa Papa Francis alivunja Taasisi ya Familia iliyoko Roma, ili kuigeuza kuwa "chombo cha kueneza nakala ya Amoris Laetitia", hati ya Francis, ambayo, kinyume na Injili, husisitiza wapokezwe Ekaristi Takatifu wazini.

Nakala hiyo imeandikwa na mhariri mkuu Thomas Jansen. Anasema kuwa Papa francis aliadhibu Taasisi Ya Familia kwani maprofesa wake walimkosoa Francis na maoni yake wakati wa Sinodi lililopita la Familia.

Kwake Jansen ni wazi kuwa Taasisi hiyo huegemea upande wa "uhifidhina", kumaanisha, Taasisi hiyo ina "Ukatoliki mwingi". Anatabiri kuwa Francis analenga kubadilisha maadili ya Kikatoliki na "maadili kulingana na hali" ambayo husemekana kuzingatia "muktadha fulani wa vitendo", badala ya kufuata sheria za kijumla na kuhukumu vitendo kulingana na hali halisi.

"Maadili ya hali" huenda yakasikika kuwa mema, lakini ukweli ni kuwa huwa yanasababisha mandhari ya maadili ya nguvu na utajiri. Ni matajiri tu ndio walio na pesa za kuibua "muktadha" ambao utaamua "kilicho adilifu na kisicho adilifu". Kupitia kwa wanahabari wao, wanadukiza "muktadha wao" katika suala lolote la maadili.

Hivyo basi ingekuwa vyema ,aidi kuzungumzia maadili ya matajiri badala ya "maadili ya hali".

Picha: © Jeffrey Bruno, Aleteia, CC BY-SA, #newsQjuzdxagwu