sw.news
28

Vita vya Wakatoliki wa Uholanzi :Maaskofu Waambiwa Wamshauri Francis

Mwezi wa Aprili tarehe tisa, wakatoliki maarufu wa Uholanzi walipeana ombi kwa maaskofu wao dhidi ya “utawala mharibifu ” wa Papa Francis, anaripoti Radio Maria Nederland. Wataalamu na makasisi wametia …More
Mwezi wa Aprili tarehe tisa, wakatoliki maarufu wa Uholanzi walipeana ombi kwa maaskofu wao dhidi ya “utawala mharibifu ” wa Papa Francis, anaripoti Radio Maria Nederland.
Wataalamu na makasisi wametia sahihi ombi hilo, baadhi yao ni daktari maarufu wa magonjwa Gerard Aardweg na Profesa wa kitambo Wilhelmus Witteman wa Chuo Kikuu cha Ufundi cha Twente.
Ombi hilo huorodhesha kashfa kubwa za Francis, zikiwemo Amoris Laetitia, kuunga kwake mkono kwa wanasiasa waliofariki Emma Bonino na Lilianne Ploumen, jitihada zake kwa kupendelea mashemasi wa kike, makasisi walioolewa na njia za kupanga uzazi, kumsifu Martin Luther King, mtazamo wake kwa Waislamu na majadiliano yake na Wakomunisti Wachina.
Ombi hilo linawasihi maaskofu wa Uholanzi kumwonya Francis katika “ wakati huu wa kuchanganyikiwa na kutojua cha kufanya ” wasifanye “makosa makubwa ” dhidi ya Imani.
Picha: © Mazur, catholicnews.org.uk, CC BY-NC-SA, #newsMylismgvot
sw.news
33

Jumapili ya Huruma :Francis Apendwa na Wanahabari Bali Aachwa na Wakatoliki

Umati mwingine uliokuwa umekerwa ulitokea wakati wa Misa ya Papa Francis ya Jumapili ya Rehema za Mungu (mwezi wa Aprili tarehe nane) katika mraba wa Mtakatifu Petro. Picha iliyowekwa hapo ilichukuliwa …More
Umati mwingine uliokuwa umekerwa ulitokea wakati wa Misa ya Papa Francis ya Jumapili ya Rehema za Mungu (mwezi wa Aprili tarehe nane) katika mraba wa Mtakatifu Petro.
Picha iliyowekwa hapo ilichukuliwa mwanzoni mwa Misa ya saa 10:30 saa za Urumi. Robo tatu za mraba ulikuwa hauna Watu.
Kanisa la Mtakatifu Spirito kule Sassia karibu na Vatikani ambayo ni Madhabahu ya Rehema za Mungu za Kirumi ilifutilia mbali Misa zote za Jumapili asubuhi ili wakristu wahudhurie Misa “iliyoongozwa ”na Francis.
#newsGxxwujlayf
sw.news
30

Fungia Huruma kwa Monsignor Capella

Monsignor Carlo Alberto Capella alipelekwa kwa jela la Vatikani mwezini wa Aprili tarehe saba kulingana na wanahabari wa Uitalia. Capella ni muunga mkono wa zamani wa Apostolic Nunciature kule Washington. …More
Monsignor Carlo Alberto Capella alipelekwa kwa jela la Vatikani mwezini wa Aprili tarehe saba kulingana na wanahabari wa Uitalia. Capella ni muunga mkono wa zamani wa Apostolic Nunciature kule Washington.
Aliitwa tena kule Roma mwezini wa Septemba mwaka wa 2017 baada ya kushtumiwa kumiliki picha za ngono za vijana. Toka hapo amekua akiishi katika jumba ambalo Vatikani inaonekana vizuri.
Kushikwa kwake wakati wa wiki ya Pasaka uliamuriwa baada ya Vatikani kupokea malalamiko rasmi kupitia njia za kidiplomasia za Marekani.
Capella anahatarisha kifungo cha jela kutoka mwaka moja hadi watano. Sasa kwa sababu yu jelani, anastahili angalau kama mgombeaji wa Papa Francis katika siku ya kuosha miguu siku ya Alhamisi Takatifu.
Picha: © Gordon, Flickr, CC BY-NC-ND, #newsYxphwssdts
sw.news
19

Kadinali Brandmüller :Mtazamo wa Wengi na Imani ya Kikatoliki ni Vitu Viwili Tofauti

Ukweli si rahisi upatikane na wengi, alisema Kadinali Walter Brandmüller katika mkutano Kanisa Katoliki, waelekea wapi? (mwezi wa Aprili tarehe saba) kule Roma. Brandmüller alisisitiza kuwa Katoliki …More
Ukweli si rahisi upatikane na wengi, alisema Kadinali Walter Brandmüller katika mkutano Kanisa Katoliki, waelekea wapi? (mwezi wa Aprili tarehe saba) kule Roma.
Brandmüller alisisitiza kuwa Katoliki sensus fidei (shahidi wa Imani kwa waumini) na “maoni ya umma” ni vitu tofauti:
“Wakati Wakatoliki en masse walizingatia hilo halali kuoa tena baada ya talaka, kutumia njia za kupanga uzazi ama vitu vingine karibu na hivyo, hii sio ushahidi wa watu wengi kwa Imani, bali kuondoka kwa wingi kutoka kwake. ”
Brandmüller pia alionyesha wasiwasi wake kwa hojaji zilizotumika kwa sinodi za hivi karibuni ya maaskofu kwani maneno ya maswali hayo yamechangia matokea kuharibiwa .
Picha: Walter Brandmüller, © Manfred Ferrari, #newsFntatuuahw
sw.news
43

Makadinali Watoa Tangazo la Imani -Lajibu Dubia

Katika mwisho wa mkutano wa Urumi “Kanisa Katoliki waenda wapi? ”(mwezi wa Aprili tarehe saba ),tangazo la mwisho lilipeanwa kwa jina la walioshiriki, wakiwemo Makadinali Brandmüller, Burke na Zen, …More
Katika mwisho wa mkutano wa Urumi “Kanisa Katoliki waenda wapi? ”(mwezi wa Aprili tarehe saba ),tangazo la mwisho lilipeanwa kwa jina la walioshiriki, wakiwemo Makadinali Brandmüller, Burke na Zen, na Askofu Athanasius Schneider.
Tangazo hilo lasema mafundisho ya Kikatoliki ya ndoa na lajibu Kadinali Dubia lilipeanwa baada ya mswada wa Francis uliozua ubishi Amoris Laetitia.
Tangazo hilo lina madokezo sita:
1. Ndoa iliyokubaliwa na kukamilishwa kati ya waja wawili waliobatizwa yaweza kuvunjwa na kifo pekee.
2. Kwa hivyo, Wakristu waliopamoja kwa ndoa halali kisha wajiunganishe na mtu mwingine wakati wenzao bado wako hai, hivyo hufanya dhambi ya mauti ya kuzinzi.
3. Hii ni amri kabisa ya kimaadili ambayo huwa ya lazima kila wakati bila kubagua.
4.. Hakuna hukumu ya raia ya dhamiri ambayo yaweza kufanya tendo mbaya liwe zuri na la haki.
5. Hukumu kuhusu ule uwezekano wa kupeana msamaha wa kisakramenti hauna msingi wa shtaka la dhambi zilizofanywa, lakini kwa nia ya anayetubu kuacha njia …More
sw.news
33

Kadinali Ampa Francis Funzo - Bila Kumtaja

Kadinali Sarah amesema kwamba "mapenzi na sheria zimeshikana". Akizungumza na kituo cha Catholic Herald (Aprili 5), alisema kwamba rafiki ya Mungu huyaheshimu mafunzo ya Mungu kulingana na maneno ya …More
Kadinali Sarah amesema kwamba "mapenzi na sheria zimeshikana".
Akizungumza na kituo cha Catholic Herald (Aprili 5), alisema kwamba rafiki ya Mungu huyaheshimu mafunzo ya Mungu kulingana na maneno ya Kristo: "Iwapo unanipenda, basi uziheshimu amri zangu."
Sarah alisisitiza kwamba makasisi na Maaskofu [akiwemo papa] hufuata ukweli huu au "wanawachanganya watu wa Mungu".
Kwa wakati mwingi Papa Francis hukashifiwa kwa kuwachanganya waumini. Pia alisema mara kadhaa kwamba ni "ugonjwa" kuifuata sheria ya Mungu "kwa kina" [soma: vyema]
Picha: Robert Sarah, © Antoine Mekary, Aleteia, CC BY-NC-ND, #newsVvvesyjwwm
sw.news
43

Msomi "Mkatoliki" Wa Masuala ya Agano La Kale Alipoteza Imani

Othmar Keel, 80, ni msomi anayejulikana kimataifa wa Agano la Kale ambaye alipata pesa nyingi kutoka kwa Kanisa Katoliki. Mlei ambaye amefunga ndoa, alifunza tangu mwaka wa 1967 hadi 2002 katika cuo …More
Othmar Keel, 80, ni msomi anayejulikana kimataifa wa Agano la Kale ambaye alipata pesa nyingi kutoka kwa Kanisa Katoliki.
Mlei ambaye amefunga ndoa, alifunza tangu mwaka wa 1967 hadi 2002 katika cuo ambacho kwa wakati mmoja kilikuwa na umaarufu cha Fribourg, nchini Uswizi.
Sasa, akizungumza mnamo Ijumaa Takatifu na gazeti la Tagesanzeiger alikiri kwamba yeye hana imani na kwamba haamini uwepo wa Mungu ambaye aliitupila mbali imani yake alipokuwa profesa "Mkatoliki".
Katika kazi yake alihusika hadharani katika kuunga mkono siasa za kihuria za Kanisa. Ni mfuasi mkuu wa chama cha Papa Francis.
Keel aliambia gazeti hilo kwamba haamini uwepo wa maisha ya baadae ila anatarajia "kurejea katika asili".
Hata hivyo, Keel anakiri kwamba yeye husali kila siku, "tabia huwa sehemu kuu ya maisha yetu ya kila siku. nisemapo Mungu, namaanisha maumbile au asili."
Baada ya kifo, Keel angetaka mwili wake utumike katika masomo ya kiafya.
Picha: Othmar Keel, © Spartanbu, wikicommons, CC BY-SA, #newsStfyaaqwgt
sw.news
33

Jumapili Ya Pasaka Yasherehekewa Kwa "Ibada Ya Mashujaa"

Parokia ya Corpus Christi katika Dayosisi ya Scranton, nchini Marekani, ilisherehekea Jumapili ya Pasaka kwa "Misa ya Mashujaa". Watoto walialikwa kuandika matendo yao mema na kuyaleta maandishi yao …More
Parokia ya Corpus Christi katika Dayosisi ya Scranton, nchini Marekani, ilisherehekea Jumapili ya Pasaka kwa "Misa ya Mashujaa".
Watoto walialikwa kuandika matendo yao mema na kuyaleta maandishi yao wakati wa misa.
Huko, maandishi hayo yaliwekwa wakati wa misa kwenye debe lililokuwa kando ya "Shujaa" wampendao zaidi".
"Mashujaa" hawa walikuwa watu ambao walikuwa wamevalia mavazi ya Superman, Batman, Wonder Woman au Super Girl.
Watoto hao waliagizwa kwamba matendo yao mema yangewasaidia "Mashujaa wetu kupata nguvu zao tena".
#newsUgfhukvhwq
sw.news
24

Mtawa Mwajentina: Francis Hukubalisha Upangaji Uzazi Bandia

Mtawa mmishonari wa shirika la Carmelite ajulikanaye Martha Pelloni, ambaye hueneza upangaji uzazi bandia, amesema kwamba Papa Francis alimwambia kwamba "uzazi wenye uajibikaji" huhitaji upangaji uzazi …More
Mtawa mmishonari wa shirika la Carmelite ajulikanaye Martha Pelloni, ambaye hueneza upangaji uzazi bandia, amesema kwamba Papa Francis alimwambia kwamba "uzazi wenye uajibikaji" huhitaji upangaji uzazi "katika hali kadhaa' [ maana kwamba: katika hali zote"].
Akizungumza na Radio Cut (Aprili 3), Pelloni alisema kwamba Francis, akizungumza naye kuhusiana na upangaji uzazi bandia, alitamka maneno matatu: "Mipira ya Kondomu, ya mpito na yanayoweza kubadilika."
Kulingana na pelloni maneno haya matatu yana maana kwamba aina tatu za upangaji uazazi bandia zimekubalishwa katika hali "kadha" [ soma:zote]: mipira ya kondomu, viwambo na "kama jambo la mwisho kabisa" kuziba mirija ya uzazi [ambalo kwa mara nyingi halibadiliki ].
Francis alikutana na Mtawa Pelloni mnamo tarehe 8 mwezi Machi mjini Rome.
Kulingana na mafundisho ya Kikatoliki matumizi ya mbinu za upangaji uzazi bandia ni hatia kubwa na ovu na dhambi ya mauti ambayo adhabu yake ni moto wa jahanamu wa milele.
Picha: Martha Pelloni, © …More
sw.news
29

Askofu Mbrazili Azungumza Katika Makao Ya Umasoni

Askofu Gilberto Pastana de Oliveira, 61, wa Crato, nchini Brazili, alitoa hotuba mnamo tarehe 14 mwezi Machi katika makao ya chama cha Freemasons ya Juazeiro do Norte. De Oliveira alisema kwamba Kanisa …More
Askofu Gilberto Pastana de Oliveira, 61, wa Crato, nchini Brazili, alitoa hotuba mnamo tarehe 14 mwezi Machi katika makao ya chama cha Freemasons ya Juazeiro do Norte.
De Oliveira alisema kwamba Kanisa na Umasoni zinaweza kuwa na uhusiano wa kidugu kwani - Kulingana naye - wengi wa wamasoni " ni Wakristo".
Kadinali Joseph Ratzinger alipokuwa Kinara wa Shirika la Mafundisho ya Imani alitoa uamuzi mnamo mwaka wa 1983 juu ya Mashirika ya kimasoni huku akisema kwamba "Maono mabaya ya Kanisa kuhusiana na shirika la umasoni hayabadiliki kwani kanuni zao zimeonekana kutolingana na mafundisho ya Kanisa na hivyo basi uanachama wake bado umepigwa marufuku."
Na, "Waumini ambao hujiunga na mashirika ya umasoni wamo katika hali ya dhambi ya mauti na hawastahili kupokea Ekaristi Takatifu."
#newsVeycmqiely
sw.news
37

"Utata Mkali" - Maaskofu Saba Wa Ujerumani Wawakana Maaskofu Wenzao Wahuria Vatikani

Kuna "utata mkali" kati ya maaskofu Wajerumani kuhusiana na kuanzishwa hivi maajuzi kwa Waprotestanti kupokea Ekariati, kituo cha Kölner Stadtanzeiger (Aprili 4) kimeripoti. Mnamo tarehe 22 mwezi …More
Kuna "utata mkali" kati ya maaskofu Wajerumani kuhusiana na kuanzishwa hivi maajuzi kwa Waprotestanti kupokea Ekariati, kituo cha Kölner Stadtanzeiger (Aprili 4) kimeripoti.
Mnamo tarehe 22 mwezi Februari, theluthi mbili za maaskofu Wajerumani "waliwakubalisha Waprotestanti kupokea Ekaristi Takatifu.
Dhidi ya uamuzi huo, maaskofu sita na Kadinali wa Cologne Rainer Woelki waliandika barua hivi maajuzi kwa, shirika la Mafundisho ya Imani na Kamati ya Umoja wa Wakristo.
Maaskofu hao sita waliuita uamuzi huo haramu, unaochukiza mafundisho ya Kikatoliki na umoja wa Kanisa. Kulingana nao, baraza la maaskofu limekidhiri uwezo wake
Picha: Rainer Maria Woelki, © Raimond Spekking, CC BY-SA, #newsJsphjnlcwz
sw.news
25

Kasisi Mchanga Azirai Wakati Wa Ibada Ijumaa Takatifu Na Kufariki

Kasisi mwenye umri wa miaka 31 Krystian Kotulski alifariki ghafla wakati wa ibada ya Ijumaa Takatifu (Aprili 30) katika kanisa la Parokia lililoko Kosobudy katika dayosisi ya Zamość-Lubaczów. Kotulski …More
Kasisi mwenye umri wa miaka 31 Krystian Kotulski alifariki ghafla wakati wa ibada ya Ijumaa Takatifu (Aprili 30) katika kanisa la Parokia lililoko Kosobudy katika dayosisi ya Zamość-Lubaczów.
Kotulski alipoteza fahamu baada ya kusambaza Ekaristi. Papo hapo alipelekwa kwenye hospitali ya John Paul II iliyoko Zamość na kuwekwa kwenye mashine za msaada wa uhai. Alifariki siku iyo hiyo saa tatu usiku. Kiini hasa cha kifo chake bado hakijajulikana.
Padre Kotulski alitawazwa miaka saba iliyopita na kutumikia kama kasisi msaidizi katika Parokia ya Mtakatifu Andrew Bobola iliyoko Kosobudy mashariki mwa Upoli.
Alikuwa kiongozi wa haji ya miguu kuelekea Czestochowa na alikuwa na wajibu wa vijana katika parokia hiyo.
Picha: Krystian Kotulski, #newsKthtkvdsop
sw.news
43

Mwanamke Adai Muujiza Wa Uponyaji Baada Ya Kuzuru Madhabahu Ya Maria

Nancy Foytik, nyanya aliyestaafu, alipatikana na kansa hatari alipozuru Madhabahu ya Kitaifa ya Bikra Maria wa Msaada Mwema huko Wisconsin, Kanisa pekee lililotambua masuka nchini Marekani. Foytik …More
Nancy Foytik, nyanya aliyestaafu, alipatikana na kansa hatari alipozuru Madhabahu ya Kitaifa ya Bikra Maria wa Msaada Mwema huko Wisconsin, Kanisa pekee lililotambua masuka nchini Marekani.
Foytik aliambia Today (Machi 28) kwamba madaktari walitarajia kwamba angefariki katika muda wa miaka miwili.
Katika Madhabahu hayo, Foytik "alihisi" sauti ikisema kwamba atakuwa salama.
Baada ya haji hiyo, alifanyiwa upasuaji lakini iapatikana kwamba Kansa hiyo ilikuwa imetoweka. Hakuna maelezo ya kimatibabu kuhusiana na suala hili ingawaje kutoweka ghafla kwa kansa ni jambo linalojulikana.
#newsHyhuribmfe
sw.news
25

Mwanaseminari Mwenye Umri Wa Miaka 30 Apatikana Amefariki Huko Rome

Anthony Freeman, 30, kutoka Lousiana, nchini Marekani, alipatikana amefariki chumbani mwake katika Seminari ya Legionaries of Christ huko Rome mnamo tarehe 2 mwezi Aprili. Alikuwa ameratibiwa kutawazwa …More
Anthony Freeman, 30, kutoka Lousiana, nchini Marekani, alipatikana amefariki chumbani mwake katika Seminari ya Legionaries of Christ huko Rome mnamo tarehe 2 mwezi Aprili.
Alikuwa ameratibiwa kutawazwa kuwa shemasi katika msimu ujao wa kiangazi.
Kiini cha kifo chake kinachunguzwa lakini kulingana na ujumbe wa Legionaries kwa wanahabari Freeman aliaga kutokana na sababu za kiasili.
Mnamo Jumapili ya Pasaka, Freeman aliubeba msalaba wakati wa Litajia ya Papa Francis huko Mtakatifu Peter.
Picha: © Anthony Freeman, regnumchristi.org, #newsWnmbwekrdv
sw.news
19

Kadinali Mhifidhina Müller ya Kadinali Mhuria Lehmann Mtakatifu

Mnamo Jumatatu ya Pasaka, Kadinali Gerhard Müller "aliongoza" huko Roma "maadimisho" ya Kiekaristi ya marehemu Kadinali wa Ujerumani Karl Lehmann. Misa Takatifu sio kwa ajili ya kuwakumbuka makadinali …More
Mnamo Jumatatu ya Pasaka, Kadinali Gerhard Müller "aliongoza" huko Roma "maadimisho" ya Kiekaristi ya marehemu Kadinali wa Ujerumani Karl Lehmann.
Misa Takatifu sio kwa ajili ya kuwakumbuka makadinali walioaga dunia ila ni ukumbusho wa mateso ya Kristo na kufufuka kwake.
Lehmann amekuwa kwa miongo mingi mharibifu katika Kanisa la Ujerumani na Kanisani kwa jumla. John Paul II aliharibu urithi wake kwa kina alipomfanya Lehmann Kadinali badala a kumharamisha.
Müller, ambaye alikuwa mwanafunzi wa Lehmann, alisema kwenye hotuba yake kwamba ana "uhakika kwamba Lehmann anatubariki kutoka binguni kwa salamu za Mtakatifu Paul". Müller alitamatisha hotuba yake kwa kusema "Kwaheri bingu".
Picha: Karl Lehmann, © Volker Jost, CC BY, #newsVijkfiqgsu
sw.news
38

Wastaarabu Wapeperusha Kiegemeo Cha Ekaristi Kanisani

Tangu Jumapili ya Pasaka video ya kinachoitwa "msafara wa Kiekaristi" katika parishi ya Gerard Majella katika dayosisi kuu ya Sorocaba, nchini Brazil, inatamba mtandaoni. Video hiyo inaonyesha kiegemeo …More
Tangu Jumapili ya Pasaka video ya kinachoitwa "msafara wa Kiekaristi" katika parishi ya Gerard Majella katika dayosisi kuu ya Sorocaba, nchini Brazil, inatamba mtandaoni.
Video hiyo inaonyesha kiegemeo cha Ekaristi kikipepea Kanisani kwa kutumia helikopta ndogo inayodhibitiwa kutoka kwa mbali.
Kasisi huyo mwenye utoto anakipokea kiegemeo hicho na kukieka kwa=enye altari.
#newsLysjzwfplu
sw.news
33

Je papa Francis Alikemewa Na Makadinali?

Antonio Socci ameandika kwenye blogu lake kwamba Papa Francis alikemewa kwa sababu ya uzushi wake kuhusiana ana jahanamu na Kadinali mmoja mkuu asiye na asili ya Kitaliano na ambaye aliwasiliana na …More
Antonio Socci ameandika kwenye blogu lake kwamba Papa Francis alikemewa kwa sababu ya uzushi wake kuhusiana ana jahanamu na Kadinali mmoja mkuu asiye na asili ya Kitaliano na ambaye aliwasiliana na makadinali wengine na kumkabili Francis pia kwa majina yao.
Socci anasema kwamba kutamka uzushi ni mojawapo wa sababu nne za kumfanya papa apoteze afisi yake.
Baada ya kukemewa, Francis alishauriana na mfuasi wake, Askofu mkuu Giovanni Angelo Becciu, msimamizi katika afisi ya Masuala ya Nchi za Kigeni.
Hili lilipelekea tangazo ambalo halikueleweka vyema la Vatikani ambalo halikuwa tatanishi kutosha, hivi kwamba, badala ya kufutilia mbali uzushi wa Francis, liliuthibitisha.
Picha: © Mazur, catholicchurch.org.uk, CC BY-NC-SA, #newsNopulvkqcp
sw.news
25

Mwanateolojia Aliyependekezwa Na Francis Ataka Kuwe na "Papa Wa Kike"

Mbenedikti mkali wa Ujerumani Anselm Grün ambaye alipendekezwa na Papa Francis mnamo tarehe 15 mwezi Februari kwa makasisi Warumi, ana imani kwamba kunaweza kuwa na "papa wa kike". Akizungumza na …More
Mbenedikti mkali wa Ujerumani Anselm Grün ambaye alipendekezwa na Papa Francis mnamo tarehe 15 mwezi Februari kwa makasisi Warumi, ana imani kwamba kunaweza kuwa na "papa wa kike".
Akizungumza na gazeti la Kijerumani Augsburger Allgemeine (Machi 31), Grün ana imani, kwamba kunaweza kuwa na makasisi, maaskofu na hata mapapa wa kike.
Grün anapendekeza kama "hatua ya kwanza" "utawazaji" wa mashemasi wa kike.
Bila shaka Grün pia anataka useja utupiliwe mbali [na hatimaye, Kanisa lote kwa jumla].
Picha: Anselm Grün, © Christlichen Medienmagazin, CC BY-SA, #newsCbnufcjpuh
sw.news
31

Utawazaji wa Wanawake Ni Suala Wazi Kwa Kadinali Wa Vienna

Suala la kuwatawaza wanawake kuwa "mashemasi, makasisi na maaskofu" linaweza tu kuamuliwa na kamati, anaamini Kadinali wa Vienna Christoph Schönborn. Akizungumza na magazeti kadhaa ya Austria (Machi …More
Suala la kuwatawaza wanawake kuwa "mashemasi, makasisi na maaskofu" linaweza tu kuamuliwa na kamati, anaamini Kadinali wa Vienna Christoph Schönborn.
Akizungumza na magazeti kadhaa ya Austria (Machi 31), Schönborn alisema kwamba Papa hawezi kuamua uteuzi wa wanawake "peke yake" ingawaje kamati pia haina nguvu za kuleta jambo kama hilo kwani linahitilafiana na Imani.
Kulingana na mafunzo ya Kanisa Katoliki wanawake hawawezi kupokea Sakramenti ya Daraja Takatifu - sawa na jinsi ambavyo wanyama hawawezi kubatizwa na jinsi ambavyo chokoleti haiwezi kuwekwa wakfu.
Kuhusiana na suala la useja wa makasisi Schönborn alisema kuna "uwezekano wa mabadiliko".
Kulingana na Schönborn, Papa Francis anataka suala hilo lijadiliwe katika sinodi la Amazon mnamo mwaka wa 2019.
Picha: Christoph Schönborn, © GuentherZ, wikicommons CC BY, #newsBlpcciaxye
sw.news
31

Askofu Mmarekani Aongoza Msafara Wa Kiekaristi Kuzunguka Kliniki Ya Uavyaji Mimba

Askofu James Conleywa Lincoln, Nebraska, aliongoza msafara wa Kiekaristi mnamo tarehe 27 mwezi Machi kutoka makao makuu ya shirika la Pro Life mjini humo kuelekea kwenye kliniki moja ya "Planned …More
Askofu James Conleywa Lincoln, Nebraska, aliongoza msafara wa Kiekaristi mnamo tarehe 27 mwezi Machi kutoka makao makuu ya shirika la Pro Life mjini humo kuelekea kwenye kliniki moja ya "Planned Parenthood".
Altari iliandaliwa kwenye bustani ya umma mbele ya mahali hapo pa maafa.
Askofu Conley ni mmoja wa nguzo za Kanisa Katoliki nchini Marekani.
Mtu anaweza kutarajia kwamba kila Askofu Mkatoliki afanye alichokifanya, lakini ni ishara ya utata mkuu uliopo Kanisani unaopeleka hali hii kutokuwepo.
#newsKhpiqszfhl