sw.news
35

"Hakuna Jahanamu" - Francis Asisitiza Urithi Wake Kama Mzushi

”Non esiste un inferno” – “Hakuna jahanamu", Papa Francis alimwambia rafikiye, mwanahabari ambaye hulipinga Kanisa Katoliki Eugenio Scalfari wa La Repubblica (Machi 28).

Francis alisema kwamba roho mbaya huwa "haziadhibiwi". Roho ambazo hutubu hupata msamaha na kuenda mbinguni, "Lakini zile ambazo hukosa kutubu na hivyo basi kukosa msamaha, hutoweka. Hakuna jahanamu. Kuna kutoweka kwa roho zenye dhambi."

Nadharia ya Francis inalingana na mafunzo ya Jehova Witnesses.

Lakini Kanisa hukiri Kwa Yesu Kristu kwamba roho ovu zitaadhibiwa kwa "moto usiozimika" na "wa milele", "ambako kutakuwa na mayowe na kusaga meno".

Kulingana na Katekisimu ya Kanisa Katoliki "Mafuzno ya Kanisa huyakinisha uwepo wa jahanamu na uwepo wake wa milele".

#newsNmnlddnokz