sw.news
49

Kauli Ya Vatikani Yathibitisha: Francis Ni Mzushi

Afisi ya utangazaji ya Vatikani ilikiri mnamo tarehe 29 mwezi Machi kwamba "Baba Mtakatifu Francis" alimkaribisha kwa mara nyingine mwanahabari mwovu Eugenio Scalfari.

Baada ya mkutano huo, Scalfari aliandika kwenye gazeti lake lipingalo Kanisa Katoliki La Repubblica kwamba Francis alikana uwepo wa jahanamu.

Afisi hiyo ya utangazaji haijapinga kwamba Scalfari aliripoti kauli ya Francis kwa njia iliyo na maudhui sahihi ila anautuliza umma kwa kusema kwamba huenda Scalfari hakuyatumia maneno halisi.

Hapo awali, Scalfari amechapisha nakala baada ya kuzungumza na Francis mnamo mwezi Septemba 2013, Julai 2014, Machi 2015, Novemba 2015 na 2016, na Julai 2017. Nakala tano kati ya zote hizi ziliibua mkano kutoka Vatikani.

Lakini mikano hii haiwezi kuchukuliwa kwa uzito kwani Francis humwalika Scalfari kila wakati ili ampe habari za kuandika kwenye nakala zake mpya.

Hivyo basi ni jambo lisilo pingika kwamba Francis huzitumia kauli zake za kutamausha kwa Scalfari ili kusababisha rabsha miongoni mwa waumini na kusababisha mzozo zaidi na utengano Kanisani

Picha: Eugenio Scalfari, © Francesca Marchi, CC BY-SA, #newsKhrhfmuvfa