sw.news
19

Kanisa Lililolala Linahitaji "Mwito" - Kutoka kwa Umormoni

Kadinali Soane Patita Paini Mafi wa Tonga na Niue, mmoja wa makadinali wanakshi wa liotolewa na Papa Francis, amesema kwenye mahojiano na kituo cha Kikatoliki (Februari 28) kuwa maendeleo ya kustaajabisha …More
Kadinali Soane Patita Paini Mafi wa Tonga na Niue, mmoja wa makadinali wanakshi wa liotolewa na Papa Francis, amesema kwenye mahojiano na kituo cha Kikatoliki (Februari 28) kuwa maendeleo ya kustaajabisha ya Umormoni huko Tonga ni "mwito" kwa Kanisa.
Dayosisi ya Kadinali huyo huwa na Wakatoliki chini ya 15,000 ambao, katika mataifa mengi, idadi hii ni ya patoko za wa wastani. Tangu mwana mdogo wa Mfalme, Prince Ata alipobadalili dini na kujiunga na Umormoni kutoka kwa umethodisti mnamo mwaka wa 2005, Umormi wa Tonga ulishuhudia maendeleo makuu na kufikia 60% ya idadi kamili ya wakazi.
Huku akimulika udhabiti wa uhubiri wa Umormoni, Mafi ana imani kuwa Kanisa inaweza kupata mafunzo kutoka kwa "matembezi ya lango kwa lango na sadaka za msaada kwa familia zinzoteseka na watu binafsi" ya Wamormoni.
Mashirika ya Kikatoliki huko Tonga, kama vile Caritas International au Jumuiya ya Mtakatifu Vincent de Paul, huwasaidia waliobaguliwa kwa kuwapa mahitaji muhimu na pia kufanya miradi ya kimazingira …More
sw.news
29

John Paul II, " Hakuna Mtu Yeyote Anayeweza Kuibadilisaha Humanae Vitae"

Profesa Stanisław Grygiel, mwenye umri wa miaka 83, mwanafalsafa Mpoli wa masuala ya maadili na rafiki wa karibu wa John Paul II, alikumbuka wakati wa wasilisho la kitabu huko Rome (Machi 7) mkutano …More
Profesa Stanisław Grygiel, mwenye umri wa miaka 83, mwanafalsafa Mpoli wa masuala ya maadili na rafiki wa karibu wa John Paul II, alikumbuka wakati wa wasilisho la kitabu huko Rome (Machi 7) mkutano wake na marehemu papa huyo. Kasisi mmoja alikuwa pamoja nao ambaye alidai kuwa ilikuwa "vigumu sana" kuishi bila mipira ya ngono na upangaji uzazi bandia.
John Paul II alimjibu, kuwa sio yeye wala Paul VI waliobuni mafundisho yaliyomo kwenye nakala ya HUmanae Vitae, "Siwezi kuyabadilisha. Hakuna anayeweza kuyabadilisha, hakuna yeyote. Hata Kanisa lenyewe haliwezi."
Grygiel aliletwa Roma na John Paul II. Alifunza katika Taasisi ya Roma Ya Masuala ya Ndoa na Familia ambayo iliuawa na Papa FRancis mnamo mwezi Septemba mwaka wa 2017.
Picha: © Jeffrey Bruno, Aleteia, CC BY-SA, #newsKzszprnigk
sw.news
28

Sababu Ya Fedha Za Vatikani Kutofanya Kazi Ni Francis

Blogu la Marco Tossatti (Februari 27) limeeleza sababu ya fedha za Vatikana kuwa katika hali ya utata: "Kwa sababu Francis hatii bidii katika kuelewa na kukagua shida; yeye husikiliza, hutoa amri kadhaa …More
Blogu la Marco Tossatti (Februari 27) limeeleza sababu ya fedha za Vatikana kuwa katika hali ya utata: "Kwa sababu Francis hatii bidii katika kuelewa na kukagua shida; yeye husikiliza, hutoa amri kadhaa na kuondoka. Kisha, anaposoma kwenye magazeti kuhusu kashfa zifuatazo kutokana na hili, hukasirika." Nakala hii imeorodhesha kutofaulu kwa Francis:
-Aliigawa wizara ya Masuala ya Nchi za Kigeni kwa kumweka Kadinali Pell kama mbabe sambamba wa kifedha ambaye hakuwa na uzoefu mwingi katika fani hiyo;
-Alimtangaza Monsignor asiye na maarifa na ambaye alijiingiza katika mambo ya kishoga Mario Battista Ricca kama mkuu wa Benki ya Vatikani, cheo muhimu ambacho kinafaa kuhakiki uhusianokati ya usimamizi wa benki hiyo na bodi la Makadinali;
-Yeye mwenyewe aliwatangaza Francesca Chaouqui na Monsignor Lucio Ángel Vallejo Baldakatika taasisi muhimu za kifedha;
-Bila kutii utaratibu unaofaa, aliwabadilisha watu kama vile Mammì na Mattietti katika usimamizi wa Benki ya Vatikani;
-Alikataa kumsikiliza …More
sw.news
39

Tena, Francis Akumbwa Na Basilika Ya Mtakatifu Peter Iliyokuwa Tupu

Papa Francis hakuwa na budi ila kukumbwa na Kanisa lililokuwa tupu kwa mara nyingine alipokuwa akisherehekea mnamo tarehe 9 mwezi Machi Ibada ya Litajia ya kutubu katika Kanisa la Mtakatifu Peter. More
Papa Francis hakuwa na budi ila kukumbwa na Kanisa lililokuwa tupu kwa mara nyingine alipokuwa akisherehekea mnamo tarehe 9 mwezi Machi Ibada ya Litajia ya kutubu katika Kanisa la Mtakatifu Peter.
Taswira sawa ilijitokeza mnamo mwezi Septemba mwaka wa 2016, ambapo Francis alisherehekea "Siku ya Maombi Duniani kwa Utunzaji wa Maumbile" ambayo hakuna mtu yeyote alijishughulisha.
Litajia hiyo ya utubu ilikuwa mwanzo wa anzilisho liitwalo "Masaa 24 ya Bwana" ambayo inahusisha kulifungua Kanisa moja katika kila Dayosisi duniani kwa maungamo kwa masaa 24 mfululizo.
#newsEmykqwpceq
sw.news
26

Jim Caviezel: "Jitengeni Na Kizazi Hiki Fisadi"

Mwigizaji Mkatoliki Jim Caviezel ambaye familia yake ina asili ya Cons/Vrin (Uswizi) na ambaye alimwiga yesu katika filamu ya The Passion of the Christ, aliwaambia wanafunzi huko Steubenville (Machi …More
Mwigizaji Mkatoliki Jim Caviezel ambaye familia yake ina asili ya Cons/Vrin (Uswizi) na ambaye alimwiga yesu katika filamu ya The Passion of the Christ, aliwaambia wanafunzi huko Steubenville (Machi 4) kwamba ni lazima wajitengr na "kizazi hiki fisadi" na "wawe mitume".
Caviezel huona vitu viwili: aitha vijana hawaogopi uovu au wanachukua "hatua ya mwisho kujitoza kwenye maelfu ya miaka gizani".
Aliongeza kuwa, "Imesemekana kuwa endapo tutashindwa katika vita hivi, na kwa kufanya hivyo, tupoteze njia zetu hizi zenye uhuru, historia itaripoti kwa kimako kikubwa, kwamba waliokuwa na vingi vya kupoteza, walifanya juhudi chache kuzuia hayo kufanyika."
Kulingana na Caviezel uhuru huwepo, "kutofanya ukipendacho, lakini kuwa na haki ya kufanya unachostahili kukifanya".
Picha: Jim Caviezel, #newsUatvcmyxje
sw.news
26

Romrero - Uwakifishaji Ulio Hatarini

Papa Francis aliidhinisha mnamo tarehe 6 mwezi Machi mwaka wa 2018 kutawazwa kwa marehemu Askofu Mkuu wa San Salvador Oscar Romero. Hata hivyo, Monsignor Jesus Delgado, Kasisi ambaye alisaidia sana …More
Papa Francis aliidhinisha mnamo tarehe 6 mwezi Machi mwaka wa 2018 kutawazwa kwa marehemu Askofu Mkuu wa San Salvador Oscar Romero.
Hata hivyo, Monsignor Jesus Delgado, Kasisi ambaye alisaidia sana katika kazi hii, aliondolewa mamlaka yake ya kichungaji mnamo mwezi Desemba mwaka wa 2016. Delgado alikuwa ndiye katibu wa Romero, mshirika wa karibu, mwandishi wa wasifu wake na msaidizi katika ombi la kutawazwa kwake.
Alikiri kuwa aliwahi kumdhulumu msichana mmoja kingono aliyekuwa na umri wa kati ya miaka 9 na 17. Hii ni kesi adimu ambapo dhulma za kijinsia zilizotekelezwa na makasisi kutokuwa ya kishoga. Mwathiriwa, aliye sasa katika miaka ya 40, aliripoti dhulma hizo kwa Serikali ya Salvador.
Ni kana kwamba dhulma hizo ziliznza punde baada ya kifo cha Romero. Mnamo mwezi Oktoba mwaka wa 2014 Delgado alikuwa mwanachama maarufu wa ujumbe kutoka El Salvador ambao ulienda Vatikani ili kumshukuru Papa Francis kwa Kutawazwa kwa Romero.
Picha: Jesus Delgado, #newsFqrbtdabbd
sw.news
24

Humanae Vitae "Haiwez Kukosolewa Na Haiwezi Kubadilika" - Kadinali Müller

Humanae Vitae ambayo hupiga marufuku upangaji uzazi bandia "haiwezi kukosolewa" kulingana na Kadinali Gerhard Müller kwani ni ya anthropologia ambayo tayari imefichuliwa na ya asili. Akizungumza wakati …More
Humanae Vitae ambayo hupiga marufuku upangaji uzazi bandia "haiwezi kukosolewa" kulingana na Kadinali Gerhard Müller kwani ni ya anthropologia ambayo tayari imefichuliwa na ya asili.
Akizungumza wakati wa sherehe ya kuwasilisha kitabu huko roma (Machi 7), Müller alisema kwamba Papa hana haja ya kutoa uamuzi kwa kutumia nguvu alizo nazo kuhusu suala hili na kuwa Papa hana nguvu za kubadilisha au kulegeza marufuku hayo.
Müller aliongeza kuwa hilo pia huwa kweli ifikapo suala la ukasisi wa wanawake ambao hauwezekani,
Picha: Gerhard Ludwig Müller, © Jolanta Dyr, CC BY-SA, #newsAxbhoooomm
sw.news
15

Seneta Wa Kwanza Mwitaliano Mwenye Asili Ya Kiafrika Achaguliwa- Vyama Viungavyo Mkono Uhamaji Havijafurahia

Toni Iwobi, mwenye umri wa miaka 62, Mkatoliki mhamaji kutoka Nigeria, amechaguliwa huko Brescia, Lombardy, kama seneta wa kwanza Mwitaliano mwenye asili ya Kiafrika katika Historia ya Jamhuri ya Italia …More
Toni Iwobi, mwenye umri wa miaka 62, Mkatoliki mhamaji kutoka Nigeria, amechaguliwa huko Brescia, Lombardy, kama seneta wa kwanza Mwitaliano mwenye asili ya Kiafrika katika Historia ya Jamhuri ya Italia. Hata hivyo, kuchaguliwa kwake hakukusifiwa na Vatikani na mashirika mengine ambayo huunga mkono uhamaji haramu.
Sababu: Iwobi ni wa chama kipingacho ihamaji haramu cha Lega Party ambacho amekuwa mwanachama wake kwa miaka 25. Chama hicho cha Lega kilikuwa chama cha pili kikuu zaidi katika bunge baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Machi. Iwobi ndiye msemaji wa chama chake juu ya mambo ya uhamaji. Alisaidia katika utunzi wa mashauri ya chama hicho yapingayoo uhamaji.
Propaganda za mrengo wa kushoto ambazo hutawala katika vyombo vikuu vya habari na ambazo hupenda kukibandika chama cha Lega taswira ya "ubaguzi wa rangi", zinashindwa kuficha mafadhaiko yake.
Picha: Toni Iwobi, #newsNbwucoqndk
sw.news
14

Jitihada Za Vatikani Kuangamiza InfoVatikana

Agosti iliyopita, Waziri wa Vatikani wa Masuala ya Nchi za Kigeni aliutishia mtandao wa Kihispania infovaticana.com kupitia kwa kampuni kubwa na maarufu ya sheria ya Baker & McKenzie. Sababu: Vatikani …More
Agosti iliyopita, Waziri wa Vatikani wa Masuala ya Nchi za Kigeni aliutishia mtandao wa Kihispania infovaticana.com kupitia kwa kampuni kubwa na maarufu ya sheria ya Baker & McKenzie. Sababu: Vatikani huwa na haki maalum ya neno 'Vatican". Hivyo basi ilitaka mtandao huo wa InfoVaticana kuisalimisha anwani yake ya infovaticana.com kwa Waziri wa Masuala ya Nchi za Kigeni wa Vatikani kwa muda usiozidi juma moja.
InfiVaticana ni mtandao bora na wenye busara zaidi ambao hukosoa utawala wa hivi sasa wa kihuria wa paleo ambao unaangamiza Vatikani. Uongozi huo ulitoa pendekezo la maafikiano ambalo lingehakikisha kuwa ghasia kati ya Vatikani na InfoVatikana zingekuwepo.
Lakini Vatikani iliambia InfoVaticana kupitia kwa kampun ya Baker & McKenzie kuwa ombi lao "halingejadiliwa" na kuwa InfoVaticana ni "lazima itoweke". Marco Tosatti alitoa maoni kwenye blogu lake, "tuna furaha kuwa katika Vatikani, angalau baadhi ya kanuni ambazo haziwezi kujadiliwa bado zipo.
Kwa wakati huu, kesi hiyo imo katika …More
sw.news
15

Ya hivi Ounde: Shujaa Mary Aachiliwa Kutoka Kwenye Jela

Mtetezi shujaa wa pro-life Mary Wagner ameachiliwa kutoka kwenye jela moja la Kanada baada ya kutamatika kwa awamu ya kwanza ya kesi yake ambayo ilianza mnamo siku ya Jumatatu. Mary alifungwa jela …More
Mtetezi shujaa wa pro-life Mary Wagner ameachiliwa kutoka kwenye jela moja la Kanada baada ya kutamatika kwa awamu ya kwanza ya kesi yake ambayo ilianza mnamo siku ya Jumatatu.
Mary alifungwa jela tangu mnamo tarehe 8, mwezi Desemba mwaka wa 2017 baada ya kuingia katika kituo cha uavyaji mimba akiwa amebeba mau nyekundu ya waridi na kuwauliza wanawake waliokuwemo kutoavya mimba yao, jambo ambalo lilipelekea kutiwa mbaroni kwa Mary mara kadhaa. Wakati kesi yake ilipokuwa ikisikilizwa, mfanyakazi mmoja kutoka kwenye kituo hicho aliulizwa iwapo uwepo wa Mary uliwahuzunisha wanawake waliokuwemo.
Mshutuko ulisikika kutoka kwa baadhi ya waliokuwa wamehudhuria kikao hicho wakati ambapo mfanyakazi huyo alijibu, "Wanawake hao huwa na huzuni kila wakati." Kesi yake itarejea mnamo tarehe 26 mwezi Aprili.
#newsChzjevzafu
sw.news
19

Papa Francis Ateua Wapinzani Wa Useja Kuandaa Sinodi La Amazon

Vatikani ilitangaza mnamo tarehe 8 mwezi Machi kuwa Papa Francis aliteua kamati ya wanachama 18 kwa matayarisho ya sinodi, kamati ambayo itaandaa sinodi la eneo la Amazon mnamo mwaka wa 2019. WAnachama …More
Vatikani ilitangaza mnamo tarehe 8 mwezi Machi kuwa Papa Francis aliteua kamati ya wanachama 18 kwa matayarisho ya sinodi, kamati ambayo itaandaa sinodi la eneo la Amazon mnamo mwaka wa 2019.
WAnachama wawili wa kamati hiyo ni wahuria wakali ambao hutetea kupigwa marufuku kwa useja, Kadinali Claudio Hummes na Askofu mzawa wa Australia aliyestaafu Erwin Kräutler.
Maandhari ya sinodi hilo pia yalitangazwa, Amazonia: njia mpya za Kanisa na za ekolojia muhimu.
Picha: Erwin Kräutler, © Holger Motzkau, CC BY-SA, #newsHunlhxwsbl
sw.news
27

Je, Bado Kuna "Utaratibu Maalum Wa Kupokewa Katika Ekaristi"? - Askofu Wa Providence

Askofu Thomas Tobin wa Dayosisi ya Providence, nchini Marekani, alianzisha kwenye mtandao wa Twitter (Machi 4) mjadala kuhusu nakala ya Amoris Laettia, Ekaristi na Dhamiri. Aliuliza "swali la kweli" …More
Askofu Thomas Tobin wa Dayosisi ya Providence, nchini Marekani, alianzisha kwenye mtandao wa Twitter (Machi 4) mjadala kuhusu nakala ya Amoris Laettia, Ekaristi na Dhamiri.
Aliuliza "swali la kweli" ambalo lilidokeza kumkosoa Papa Francis kama: "Iwapo dhamiri ya mtu ndio utaratibu ambao hutumika kumpokeza mtu Ekaristi, je, hili hutumika pia kwa Sakramenti zinginezo? Hata Daraja Takatifu?"
Au: "Bado kuna utaratibu maalum wa kupokewa katika Sakramenti katika Kanisa Katoliki?"
Picha: Thomas Joseph Tobin, © Jim Forest, CC BY-NC-ND, #newsEwvnvtfpnp
sw.news
23

Maaskofu Wajerumani, Kuzibariki Ndoa Za Kishoga Ni Dhidi Ya Injili

Kanisa halina "uhuru" wa kubariki husiano za kishoga, Askofu Msaidizi Dominikus Schwaderlapp alisema mjini Cologne, nchini Ujerumani. Akizungumza na Die Tagespost (Machi 8), Schwaderlapp alisema kuwa …More
Kanisa halina "uhuru" wa kubariki husiano za kishoga, Askofu Msaidizi Dominikus Schwaderlapp alisema mjini Cologne, nchini Ujerumani.
Akizungumza na Die Tagespost (Machi 8), Schwaderlapp alisema kuwa kuwabariki wenzi shoga kutakuwa na maana kuwa "kujitenga na Injili". Kulingana na Schwaderlapp, Kanisa halistahili kubariki uhusiano wowote ambao huhusisha vitendo vya ngono nje ya ndoa.
Kauli ya Schwaderlapp huenda haina maana yoyote kwani Maaskofu wanajulikana kuichanganya imani ya Kikatoliki na maoni ya kibinafsi ambayo wanaweza kuyabadilisha kulingana na wakati.
#newsSuxuwswzhj
sw.news
28

Kadinali Brandmüller: Maaskofu Wajerumani "Wenye Uwongo Mwingi"

Jitihada la Maaskofu Wajerumani kuwakubalisha Waprotestanti Wajerumani kupokea Ekaristi katika "kesi binafsi" ni "hatua ya busara" ili kuingiza Ekaristi kwa Wasio wakatoliki, Kadinali Walter Brandmüller …More
Jitihada la Maaskofu Wajerumani kuwakubalisha Waprotestanti Wajerumani kupokea Ekaristi katika "kesi binafsi" ni "hatua ya busara" ili kuingiza Ekaristi kwa Wasio wakatoliki, Kadinali Walter Brandmüller, mwenye umri wa miaka 89, aliyebadili dini kutoka kwa uptrotestanti.
Akizungumza na kituo cha Austria kath.net (Machi 6), Brandmüller alionyesha kuwa Maaskofu Wajerumani hutumia "ujuzi wa kisalami" na kuliita "uongo mtupu"
Kulingana na Kadinali huyo, kadirio la Maaskofu Wajerumani kwamba kuna Waprotestanti walio na nja ya Kiekaristi wanaohitaji usaidizi, "Hadithi iliyotungwa kimaksudi, badalaya Kkitsch". Brandmüller huuliza swali mbona Waprotestanti hao wa maaskofu Wajerumani hukosa kubadili dini na kuwa Wakatoliki.
Picha: Walter Brandmüller, © Manfred Ferrari, #newsVmhsbqooqc
sw.news
30

Watawa Wafaransa Wadhulumiwa Na Vatikani

Watawa arobaini wa kutafakari wa shirika la Little Sisters of Mary, Mama ya Mkombozi, mjini Saint-Aignan-sur-Roe, nchini Ufaransa, hudhulumiwa na askofo wao mhuria Thierry Scherrer wa Laval, kulingana …More
Watawa arobaini wa kutafakari wa shirika la Little Sisters of Mary, Mama ya Mkombozi, mjini Saint-Aignan-sur-Roe, nchini Ufaransa, hudhulumiwa na askofo wao mhuria Thierry Scherrer wa Laval, kulingana na taarifa za riposte-catholique.fr (February 27).
Watawa hao wana makao manne ya kuwatunza wazee na hapo awali walifanya kazi katika nyumba ya askofu. Scherrer huwaona watawa hao "kuwa watamaduni zaidi". Amekasirishwa haswa na kuwa watawa hao waliamua wakati wa kongamano lao kuu mnamo mwaka wa 2012 kuzirejelea tabia za zamani.
Baada ya kuunganishwa kwa makao hao ya kuwatunza wazee, Scherrer amekuwa mwanachama wa bodi simamizi ya shirika la umma ambalo huyatawala makao hayo. Hakuna mtaalamu, alidukiza maamuzi ya usimamizi bila kusikiliza ushauri wowote wa kitaalam. Huku akikumbwa na upinzani kutoka kwa watawa hao aliamuru ziara ya kichungaji ambayo matokeo yake yalikuwa tayari yameamuliwa.
Scherrer alilihusisha shirika la Dini ambalo lilibandua baraza la watawa hao na kuwahamisha Mkurugenzi …More
sw.news
27

Kadinali Mzushi Kasper Akiri Kwamba Uzushi Umempofusha

Mjadala Kuhusu nakala ya Amoris Laetitia "una madai mengi ya kizushi", Kadinali Walter Kasper anaamini. Akizungumza na mtandao wa vaticannews.va (Machi 5), Kasper alidai kuwa Papa Francis hajatilia …More
Mjadala Kuhusu nakala ya Amoris Laetitia "una madai mengi ya kizushi", Kadinali Walter Kasper anaamini.
Akizungumza na mtandao wa vaticannews.va (Machi 5), Kasper alidai kuwa Papa Francis hajatilia shaka udhabiti wa ndoa [ingawaje bila shaka aliifutilia mbali] .
Wakati wa mahojiano hayo, Kasper mwenyewe alitamka uzushi alipodai kuwa si bayana iwapo wazini huwa wakitenda dhambi au la. Kulingana naye baada ya uzini "dhamiri inafaa kuchunguzwa kindani ndani iwapo bila shaka kuna dhambi kuu, au pengine dhambi inayoweza kusameheka, au pengine pasiwe na chochote." Madai haya yanahitilafiana vikali na mafunzo ya Papa wote waliomtangulia Francis.
Kwa kudata vikali katika uzushi, Kasper anakiri kwamba haoni sababu yoyote ya Ekaristi kwa wazini ni Uzushi.
Picha: Walter Kasper, © Mazur, catholicchurch.org.uk, CC BY-NC-SA, #newsSaeflzbfha
sw.news
34

Kadinali Mwafrika: Kanisa La Bara Uropa Linafaa Kupambana Na Makanisa Yaliyotupu, Sio Ushoga

Kadinali John Onaiyekan wa Abuja, nchini Nigeria, ameeleza kustaajabishwa kwake na Kanisa Katoliki barani Uropa linavyojishughulisha na ushoga linapostahili kuwa likijalishwa na makanisa na seminari …More
Kadinali John Onaiyekan wa Abuja, nchini Nigeria, ameeleza kustaajabishwa kwake na Kanisa Katoliki barani Uropa linavyojishughulisha na ushoga linapostahili kuwa likijalishwa na makanisa na seminari zao kuwa tupu.
Akizungumza na kituo bandia cha habari cha Australia orf.at (Machi 2), Onaiyekan alisema kuwa mafunzo ya Kanisa juu ya ushoga yako wazi na kuwa ushoga hauwezi kuidhinishwa, "Hili haliwezi kubadilishwa."
Suala a ushoga tayari limeibua utengano katika ushirika wa Kianglikani. Sasa, inaonekena kwamba Papa Francis anataka kulete utengano sawa na huo katika Kanisa Katoliki.
Picha: John Onaiyekan, © IPP FoRB, CC BY-NC, #newsSbsgavkmss
sw.news
69

Waseminari Wa Zamani Wamkengemeka Askofu Wa Hondura Kwa Madai Ya Uzini Wa Kishoga

Edward Pentin amepata ushuhuda zaidi kutoka kwa waseminari wa zamani wa Dayosisi kuu ya Tegucigalpa, Honduras, kuhusu uzini wa kishoga wa Askofu Msaidizi Juan Pineda. Ushahidi huo uliandikiwa upelelezi …More
Edward Pentin amepata ushuhuda zaidi kutoka kwa waseminari wa zamani wa Dayosisi kuu ya Tegucigalpa, Honduras, kuhusu uzini wa kishoga wa Askofu Msaidizi Juan Pineda. Ushahidi huo uliandikiwa upelelezi wa Vatikani uliofanywa na Askofu wa Argentina Alcides Casaretto mnamo mwezi mwaka wa 2017. Tangu wakati huo yamekuwa mikononi mwa Papa Francis.
Dayosisi kuu ya Tegucigalpa huongozwa na Kadinali Oscar Rodríguez Maradiaga, rafiki wa karibu wa Francis na rafiki wa Pineda. Pineda amekuwa kiongozi wa dayosisi hiyo tangu mwezi Januari, kwani Rodríguez hupata matibabu ya kemikali mjini Houston, Texas, kutibu kansa ya tezi-kibofu.
Ushahidi huo una matukio ambayo husemekana yalitendeka wakati Pineda alipokuwa 9akifunza katika seminari. Baadae waseminari hao wawili wa kitambo walilazimika kutoka katika seminari hiyo. Kulingana na shahidi wa kwanza, Pineda alijaribu kuwa na uhusiano wa kingono, "Usiku alikuja karibu nami na kuzishika sehemu zangu za siri na vile vile kifua, nilijaribu kumwachisha,…More
sw.news
45

Uchaguzi Wa Italia: Papa Francis Na Vyama Vya Mrengo Wa Kushoto Washindwa

Chama cha zamani cha Kikomunisti nchini Italia, Partito Democratico (PD), ambacho serikali yake ilikuwa uongozini tangu mwezi Machi mwaka wa 2013, kilishindwa katika uchaguzi mkuu wa jana, huku kikipokea …More
Chama cha zamani cha Kikomunisti nchini Italia, Partito Democratico (PD), ambacho serikali yake ilikuwa uongozini tangu mwezi Machi mwaka wa 2013, kilishindwa katika uchaguzi mkuu wa jana, huku kikipokea chini ya 20% ya kura. Chama hiki ndicho kilichoongoza serikali iliyopinga Kanisa Katoliki zaidi katika historia ya jamhuri ya Italia.
Serikali hiyo ya PD ilichochea uhamaji haramu na kuingiza ndoa za kishoga na kifo kisicho na maumivu, hata hivyo, serikali hiyo ilikuwa na upendeleo dhabiti wa Papa Francis.
Wakati ambapo Wakatoliki milioni mbili walipokusanyika huko Roma mnamo mwezi Januari mwaka wa 2016 kuipinga serikali hiyo ambayo ilikuwa inaelekea kuingiza ndoa za kishoga, Bergoglio aliwapuuza kabisa waandamanaji. Pia alibaki kimya wakati ambapo serikali ya mrengo wa kushoto iliingiza kifo kisicho na maumivu. Badala yake alifariji kwa shauku misimamo ya serikali hiyo ya kupendelea uhamaji haramu.
Mmoja wa majabari wa Francis katika siasa za Kitaliano ni Emma Bonino, ambaye huwa mwovu …More
sw.news
20

Kadinali Kaspe Ataka Kutumia "Kitimbi Cha Kesi Moja Peke Yake" Katika Ekaristi Na Ukasisi

Akizungumza na mtandao wa Maaskofu Wajerumai katholisch.de (Machi 4), Kadinali wa Kisasa Walter Kasper alidai bila kicheko kuwa Kanisa Katoliki "limekaribia sana" ufahamu wa Kiluther juu ya Ekaristi …More
Akizungumza na mtandao wa Maaskofu Wajerumai katholisch.de (Machi 4), Kadinali wa Kisasa Walter Kasper alidai bila kicheko kuwa Kanisa Katoliki "limekaribia sana" ufahamu wa Kiluther juu ya Ekaristi na ukasisi.
Alipendekeza matumizi ya "kitimbi cha kesi moja peke yake" ambayo yamewapendeza watu wengi chin ya Papa Francis na ambayo huenda yakakubalisha kutupiliwa mbali kwa Ekaristi ya Kikatoliki pamoja na ukasisi wa Kikatoliki.
Tayari Papa Francis ametumia "kitimbi cha kesi moja peke yake" ili kutambua talaka Kanisani. Hili halijasababisha umoja na Waprotestanti ila limesababisha utengano mkuu Kanisani kati ya wachungaji wahuria na familia za Kikatoliki hivi kwamba Papa Francis anaweza kuitwa papa wa farakano wa karne ya 21.
Picha: Walter Kasper, © Mazur, catholicchurch.org.uk, CC BY-SA, #newsYyngypdzco