sw.news
43

Benedict Akashifu “Theology of Pope Francis”

Hatimaye barua kamili imechapishwa ambayo Benedict XVI alimwandikia Monsignor Dario Viganò, Afisi ya Mawasiliao ya Vatikani, kama jibu la ombi la kuandika utangulizi wa vitabu kumi na kimoja viitwavyo …More
Hatimaye barua kamili imechapishwa ambayo Benedict XVI alimwandikia Monsignor Dario Viganò, Afisi ya Mawasiliao ya Vatikani, kama jibu la ombi la kuandika utangulizi wa vitabu kumi na kimoja viitwavyo “Theology of Pope Francis”(
Teolojia ya Papa Francis). Kupitia kwa barua hiyo yake, Benedict alikataa ombi hilo kwa heshima.
Mapema juma hili Viganò alichapisha sehemu zilizokuwa zimechaguliwa za barua hiyo, sehemu ambazo ziliashiria kwamba Benedict alikuwa amemsifu Feancis na "Teolojia" yake.
Sehemu za barua hiyo ambazo hazikuchapishwa hapo awali na kisha kuchapishwa hivi maajuzi zinashambulia kwani Benedict XVI alikosoa kuwa Mwanateolojia Mjerumani Padre Peter Hünermann ambaye hulipinga Kanisa yumo miongoni mwa waandishi wa vitabu hivyo. Hivi ndivyo alivyoandika Benedict:
"La ziada ningetaka kueleza mshangao wangu kwa kuwa miongoni mwa waandishi yupo Profesa Hünermann, ambaye wakati wa Upapa wangu alijitambulisha kwa kuongoza miradi dhidi ya Papa. Alishiriki pakubwa katika uchapishaji …More
sw.news
24

Kuna Ushahidi Kwamba Kadinali Schönborn Alidanganya

Marco Ansaldo aliripoti wakati wa Sinodi la Famiia mnamo mwaka wa 2015 kuwa Benedict XVI alikuwa amemwalika Kadinali Schönborn wa vienna kushirirki chakula cha mchana ili kumhimiza aandae mkutano wa …More
Marco Ansaldo aliripoti wakati wa Sinodi la Famiia mnamo mwaka wa 2015 kuwa Benedict XVI alikuwa amemwalika Kadinali Schönborn wa vienna kushirirki chakula cha mchana ili kumhimiza aandae mkutano wa maridhiano kati ya Kadinali Müller na Kadinali Kasper.
Msemaji wa Schönborn alikana ripoti hiyo kwa kituo cha onepeterfive.com (Februari 3) huku akidai kuwa ripoti hiyo ya Ansaldo ilikuwa "uwongo mtupu".
Lakini mnamo tarehe 212 mwezi Machi kituo cha onepeterfive.com kilitangaza kuwa kilizungumza mnamo mwezi Januari na wasemaji wengine ambao waliunga mkono ripoti hiyo ya Ansaldo. Wasemaji wawili ambao hawakujitambulisha ambao walikuwa wanachama wa kikundi kilichozungumza Kijerumani katika sinodi hilo la mwaka wa 2015, walidhihirisha kwamba bila shaka mkutano kati ya Schönborn na Benedict ulifanyika.
Msemaji mmoja alisema kwamba ripoti ya Ansaldo ilikuwa sahihi katika maudhui yake na kwamba mkutano huo ulikuwa "wazi sana kwa kikundi hicho kizungumzacho Kijerumani". Ansaldo alishikilia msimamo …More
sw.news
22

Dayosisi Ya Kitaliano, Wazini Wanaweza Kuwa Wadhamini Wa Ubatizo, Waalimu Wa Dini Na Wakatekisti

Askofu Marcello Semeraro wa Albano, nchini Italia, amejitwika juu ya Injili na kuagiza kuwa wazini wanaweza kupokea Ekaristi takatifu na pia kuchukua majukumu ya uongozi katika dayosisi yake. Semeraro …More
Askofu Marcello Semeraro wa Albano, nchini Italia, amejitwika juu ya Injili na kuagiza kuwa wazini wanaweza kupokea Ekaristi takatifu na pia kuchukua majukumu ya uongozi katika dayosisi yake. Semeraro ni rafikiye Francis na pia katibu katika baraza lake la Makadinali. Agizo lake lina jina la kitoto "Furahia nami" na lina msingi wa Amoris Laetitia.
Kulingana na kituo cha SIR, Semeraro huwakubalisha wazini kusoma Biblia wakati wa Ibada Takatifu, kuwa waalimu wa dini katika mashule na wakatekisti katika paroko. Huwa anawalazimisha makasisi wake kutowahimiza wazin kuishi utakatifu utakatifu endapo hilo huwazidi "nguvu".
Kamati ya Trent ilikashifu uzushi ambao ulidai kwamba haiwezekani kuzitii amri za Mungu. Hivyo basi makasisi katika dayosisi yake watatenda dhambi endapo watamfuata Semeraro.
Picha: Marcello Semeraro, #newsFjqnrpblqe
sw.news
25

Askofu Mkuu Wa Guam Apatikana Na Makosa Ya Dhulma Za Kishoga

Tume ya majaji watano wa Vatikani wamempata Askofu Mkuu Anthony Apuron na makosa ya kuwadhulumu kishoga vijana wa kiume miongo iliyopita. Tume hiyo ilitangaza uamuzi wake katika ujumbe kwa wanahabari …More
Tume ya majaji watano wa Vatikani wamempata Askofu Mkuu Anthony Apuron na makosa ya kuwadhulumu kishoga vijana wa kiume miongo iliyopita. Tume hiyo ilitangaza uamuzi wake katika ujumbe kwa wanahabari (Machi 16).
Apuron "alipatikana na baadhi ya makosa aliyodaiwa kuyafanya". Ataadhibiwa kwa kung'atuliwa afisini na kupigwa marufuku dhidi ya kuishi kwenye kisiwa cha Guam.
Jaji aliyekuwa akiyaongoza mashtaka hayo alikuwa Kadinali Raymond Burke, mtaalam katika sheria ya Kanisa.
#newsHhmmpedogd
sw.news
26

Vatikani Yaita Hitilafu "Sanaa"

Kituo cha habari cha Kitaliano ANSA kilipata uhondo kutoka kwa "wasemaji wakuu katika Vatikani" kwamba "hakukuwa na hitilafu" katika barua ya Benedict XVI iliyochapishwa kwa mapendeleo ambapo Benedict …More
Kituo cha habari cha Kitaliano ANSA kilipata uhondo kutoka kwa "wasemaji wakuu katika Vatikani" kwamba "hakukuwa na hitilafu" katika barua ya Benedict XVI iliyochapishwa kwa mapendeleo ambapo Benedict alitoa maoni kuhusiana msururu wa vitabu vilivyoandikwa kwa ajili ya "Teoloji" ya Papa Francis.
Kuna uwezekano mkubwa kwamba msemaji huyo ni mshukiwa mwenyewe, Monsignor Dario Edoardo Viganò, kinara wa Sekretarieti ya Mawasiliano.
Msemaji huyo alidai kuwa picha iliyochapishwa na kituo cha VaticanNews "bila shaka ni yenye usanii mwingi" huku akiongeza kuwa sehemu ambazo hazikusomeka alizisoma Monsignor Viganò wakati wa kikao na wanahabari. Hata hivyo, kituo cha AP kilitanga mnamo siku ya jumatano, kwamba Vatikani "ilikiri" kuhitilafiana na picha hiyo kumaanisha kuwa ukiukaji wa viwango vya wanahabari.
Picha: Dario Edoardo Viganò, © Associazione Amici di Piero Chiara, CC BY, #newsVnbvfhzllo
sw.news
18

Inasemakana Kuwa Papa Francis "Huteseka"

Waandishi wanapoonyesha kuwa Francis anayasaliti mafundisho ya Kanisa basi inasemekana kuwa Francis "huteseka" kulingana na Askofu Mkuu Angelo Becciu, kaimu katika Waizara ya Masuala ya Nchi za Kigeni …More
Waandishi wanapoonyesha kuwa Francis anayasaliti mafundisho ya Kanisa basi inasemekana kuwa Francis "huteseka" kulingana na Askofu Mkuu Angelo Becciu, kaimu katika Waizara ya Masuala ya Nchi za Kigeni ya Vatikani, na mfuasi ambaye huwa hakosoi chochote Francis akisemacho wala kukifanya.
Becciu aliambia kituo cha Rome Reports (Machi 14) kuwa utafiti wa aina hiyo "hufika moyoni mwa mtu" na kuwa hili ni "shutuma kali zaidi ambazu anaweza kuzipata" [kama Papa].
Kauli hii ni ya kweli kabisa.
Picha: Angelo Becciu, © UK in Holy See, CC BY-NC, #newsPaqjfylzam
sw.news
25

Kadinali Mzee Kasper: Waprotestanti Ni Sawa Na Uzini Wa Kishoga

Uzini wa kishoga - ambao kulingana na Biblia ni "la kuchukiza"- unaweza kupata kwa mapendeleo na mfanano sifa za ndoa ya Kikristo, Kadinali ambaye bila shaka ni mzee Walter Kasper, mwenye umribwa miaka …More
Uzini wa kishoga - ambao kulingana na Biblia ni "la kuchukiza"- unaweza kupata kwa mapendeleo na mfanano sifa za ndoa ya Kikristo, Kadinali ambaye bila shaka ni mzee Walter Kasper, mwenye umribwa miaka 85.aliandika kwenye kitabu kipya juu ya Amoris Laetitia.
Kasper ana imani kuwa ndoa na uzini wa kishoga ni kama Wakristo Wakatoliki na Wakristo wasio Wakatoliki, "Kwani kuna sifa nje ya Kansia Katoliki sifa za Kanisa la kweli, katika husianl zilizotajwa hapa juu [uzini wa kishoga, uzini] kunaweza kuwa na sifa zilizoko katika ndoa ga Kikrist, ingawaje hazitimizi ubora kwa ukamilifu."
Kadinali Ratzinger aliandika alipokuwa kinara wa Shirika la Mafundisho ya Imani mnamo mwaka wa 2003, kwamba" hakuna mizingi kamwe ya kufikiria kuhusu uhusiano wa kishoga [uzini wa kishoga] kuwa kwa njia yoyote ile sawa na mpango wa Mungubwa ndoa na Familia. "
Na," Ndoa ni takatifu, huku vitendo vya kishoga huwa dhidi ya sheria za asili za maadili. "
Picha: Walter Kasper, © Mazur/catholicchurch.org.uk, CC BY-NC-SAMore
sw.news
27

Jinsi Ambavyo Gloria.tv Hudhaminiwa

Gloria.tv haina waajiriwa wowote na licha ya hilo, ni mtandao mkubwa zaidi na huwa na wafuasi wengi zaidi kushinda baadhi ya mitandao ya kibiashara ya Kikatoliki. Huwa tunailinda Imani Katoliki na hili …More
Gloria.tv haina waajiriwa wowote na licha ya hilo, ni mtandao mkubwa zaidi na huwa na wafuasi wengi zaidi kushinda baadhi ya mitandao ya kibiashara ya Kikatoliki. Huwa tunailinda Imani Katoliki na hili linavutia idadi inayokuwa kwa kasi ya wafuasi, haswa marekani ya Kusini.
Gloria.tv sio biashara, ni kazi ya uhubiri. Hata hivyo, huwa na gharama za ufanyakazi ambayo huwa kubwa kwetu (takriban dola 100,000 mnamo mwaka wa 2017). Tofauti na vituo vya habari vya kihuria vya "Kikatoliki" hatuna wadhamini mabwenyenye ili kueneza itikadi za kihuria. Gloria.tv hutegemea tu mchango kutoka kwa Wakatoliki binafsi.
Iwapo kuna jinsi unavyoweza kutusaidia, tafadhali tusaidie. Tunauhitaji usaidizi wako ili kuendeleza Utume mkubwa na unaoendelea kukua wa Kikatoliki kwenye mitandao ya Intaneti.
Tafadhali, tusaidie wakati huu wa Kwadrajesma
#newsSfuypiitcl
sw.news
18

Uhuria Wa Francis Waleta Viti Vitupu Kanisani - Vatikani Yazificha Idadi

Vatikani huchapisha mnamo mwezi Desemba idadi za wageni ambao huhudhuria mikutano ya mikutano ya hadharani ya Francis (Litajia, hotuba, Angelus) za mwaka huo. Lakini mnamo mwezi Desemba mwaka wa 2017 …More
Vatikani huchapisha mnamo mwezi Desemba idadi za wageni ambao huhudhuria mikutano ya mikutano ya hadharani ya Francis (Litajia, hotuba, Angelus) za mwaka huo. Lakini mnamo mwezi Desemba mwaka wa 2017 hili halikufanyika. Katika miaka ya hivi maajuzi idadi hizi zimekuwa zikipungua sana:
2014: Wageni milioni 5.92
2015: Wageni milioni 3.21
2016: Wageni milioni 3.95
2017: ???
Idadi ya wahaji ambao huwa na haja ya kumwona Papa Francis wakati wa Hotuba ya Jumla ya Jumatano zinatamausha zaidi:
2014: Milioni 1.2
2015: Milioni 0.7 2016: Milioni 0.8 2017: ??? Hili lilikuwa sawa wakati wa ziara ya Francis nchini Chile. Kulingana na kituo cha usnews.com umati ulikuwa "mkonde sana, katika baadhi ya maeneo kulikuwa na mstari moja tu wa watu." Picha: © Mazur/catholicnews.org.uk, CC BY-NC-SA, #newsEzwdclaisp
sw.news
25

Vatikani Ilivuta kwa Hari Picha Ya Barua Ya Benedict

Kituo cha Associated Press kiliripoti mnamo tarehe 14 mwezi Machi kuwa Monsignor Dario Edoardo Viganò, kinara wa Sekretarieti ya Mawasiliano, alikiri kuvuta kwa hira barua kutoka kwa Benedict XVI. …More
Kituo cha Associated Press kiliripoti mnamo tarehe 14 mwezi Machi kuwa Monsignor Dario Edoardo Viganò, kinara wa Sekretarieti ya Mawasiliano, alikiri kuvuta kwa hira barua kutoka kwa Benedict XVI.
Mnamo mwezi Januari, Viganò alimtumia Benedict sehemu kumi na moja za nakala zilizoandikwa na Padre Roberto Repole kuhusiana na umuhimu wa kiteolojia wa Papa Francis, huku akimuuliza Benedict kuchangia ukurasa wa kiteolojia kwa sehemu hizo. Lakini Benedict alimjibu:
"Kwa bahati mbaya, ingawaje kwa sababu za kimwili, sina uwezo wa kuzisoma sehemu hizo kumi na moja katika wakati ujao, zaidi kwa sababu nina majukumu mengine ambayo tayari nimeyachukua."
Mnamo siku ya Jumatatu, Viganò alichapisha picha ya barua hiyo ya barua ya Benedict XVI ikionyesha sehemu fupi ambapo benedict, kwa ajili ya upole, anataja sifa kwa "teolojia ya Francis". Sehemu hiyo nyengine ya barua hiyo, haswa nukuu iliyo hapa juu, ilifichwa.
Dondoo hiyo iliyochapiswa na Viganò ilipendekeza kuwa Benedict alikuwa amesoma vitabu …More
sw.news
22

Francis Husema Chochote Anachoamini Wasikilizaji Wake Wangetaka Kusikia

Papa Francis aliwaambia wahaji Wapoli mwishoni mwa Hotuba yake Kuu mnamo tarehe 14 mwezi Machi kwamba yeyote ambaye ametenda dhambi ya mauti anastahili kupokea ondoleo la dhambi katika Sakramenti ya …More
Papa Francis aliwaambia wahaji Wapoli mwishoni mwa Hotuba yake Kuu mnamo tarehe 14 mwezi Machi kwamba yeyote ambaye ametenda dhambi ya mauti anastahili kupokea ondoleo la dhambi katika Sakramenti ya Upatanisho kabla ya kupokea Ekaristi. Hili halilingani na nakala yake ya Amoris Laetitia wala na alichokisema alipokuwa akilizuru kanisa la Kiluther huko Roma.
Wahaji Wajerumani aliowalisha badala yake kwa upuzi mtupu: "Kwa mwongozo wa wema wa Bwana na tukiwa na matumaini takatifu si haba, tunaweza pia kuwaonyesha ndugu zetu mapenzi ambayo Mungu hutupa kila siku."
#newsUadjybaacx
sw.news
35

Mtakatifu Bridget: Papa Ambaye Atatupilia Mbali Useja Watakuwa Chakula Cha Shetani Huko Jahanamu

Wakati ambapo Mtakatifu Bridget wa Uswidi, +1373, alikuwa mjini Naples, nchini italia, kama mshauri wa Askofu Mkuu Bernado wa Naples, kwa wakati mmoja walizungumza kuhusu Makasisi kuishi na wanawake. …More
Wakati ambapo Mtakatifu Bridget wa Uswidi, +1373, alikuwa mjini Naples, nchini italia, kama mshauri wa Askofu Mkuu Bernado wa Naples, kwa wakati mmoja walizungumza kuhusu Makasisi kuishi na wanawake. Bernado alitoa hoja kuwa, iwapo alikuwa papa, angefutilia mbali useja ili kuepukana na kashfa za aina hiyo.
Mtakatifu Bridget alimjibu kuwa Bikra Maria alimwambia (Ufunuo, kitabu cha 7, Kichwa cha 10) kuwa Papa atakatupilia mbali useja "ataondolewa maono yake ya kiroho pamja na uwezo wake wa kusikia kiroho na Mungu" na "maarifa yake ya kiroho yatakuwa baridi kwabisa."
Bikra Maria aliongeza kuwa "baada ya kifo chake, roho yake itatupwa nje na kuteswa daima na milele huko jahanamu ambako itakuwa chakula cha shetani daima na bila kikomo."
Picha: Heliga Birgitta, © Lawrence OP, CC BY-NC-ND, #newsQjelgrjrnl
sw.news
32

Watawa Wafransisko Wa Bikra Maria Waungana Tena - Kama Wanawake Wacha Mungu

Inasemekana kuwa Watawa Wafransisko wa Bikra Maria ambao walifukuzwa na Vatikani kutoka kwenye shirika hio, wanaungana tena, kulingana na blogu la Veritacommissariamentoffi ambalo hueneza chuki dhidi …More
Inasemekana kuwa Watawa Wafransisko wa Bikra Maria ambao walifukuzwa na Vatikani kutoka kwenye shirika hio, wanaungana tena, kulingana na blogu la Veritacommissariamentoffi ambalo hueneza chuki dhidi ya watawa hao.
Mpango wa Watawa hao ni kuunda jumuia ya umma kwa waumini. Hili litawawezesha kuepukana na dhulma ambazo hutekelezwa na Shirika la vatikani la Waumini. Watawa wamezichukua tabia na wanarejea kwenye makao yao ambayo walilazimika kuyaacha kwa ajili ya utiifu. Vatikani haina nguvu juu ya makao hayo kwani yanamilikiwa na jumuia ya huru ya walei.
Hivi watawa hao wameweza kurejea kwenye makao yao ya Frigento, katika jengo lililoko Giovanni Rotondo, pahali ambapo Padre Pio alifariki, na kwenye madhabahu yaliyoko Mlimani Gargano.
#newsVeawahzzdg
sw.news
24

Kadinali Mjinga Mhispania Aliunga Mkono Waandamanaji Ambao Walilishambuli Makanisa

Waandamanaji ambao huunga mkono uavyaji mimba walichafua Makanisa mawili ya Katoliki katika Dayosisi kuu ya Madrid kama sehemu ya sherehe za Siku ya Wanawake ya Kimataifa (Machi 8). Waliandika maandishi …More
Waandamanaji ambao huunga mkono uavyaji mimba walichafua Makanisa mawili ya Katoliki katika Dayosisi kuu ya Madrid kama sehemu ya sherehe za Siku ya Wanawake ya Kimataifa (Machi 8). Waliandika maandishi ya ukufuru kwenye kuta za Makanisa ya Espíritu Santo na San Cristóbal.
Kabla ya shambulizi hilo, Kadinali wa Madrid Carlos Osoro aliwaunga mkono waandamanaji hao walipingalo Kanisa, huku akidai kwa ukufuru, "Bikra Maria angejiunga na waandamanaji hao".
Kinyume na hayo Askofu wa San Sebastian Ignacio Munilla alikashifu maandamano hayo kwa sababu ya itikadi za mkutano huo za kijinsia ambazo - alieleza -, "zilichukuliwa chini ya ushawishi wa shetani."
#newsDzhhpflfki
sw.news
29

Maaskofu Watatu Ni Wanachama Wa Kongamano La Kitaifa La Uchina

Kulikuwa na Maaskofu watatu miongoni mwa wajumbe wa Kongamano la 13 la Kitaifa la Uchina ambalo mnamo tarehe 11 liliamua kuidhinisha muhula usioisha katika ofisi ya rais wa Uchina, kulingana ana kituo …More
Kulikuwa na Maaskofu watatu miongoni mwa wajumbe wa Kongamano la 13 la Kitaifa la Uchina ambalo mnamo tarehe 11 liliamua kuidhinisha muhula usioisha katika ofisi ya rais wa Uchina, kulingana ana kituo cha AsiaNews (Machi 13)
Wa kwanza Joseph Huang Binvzhang, askofu wa Shantou aliyeteuliwa na serikali na ambaye aliharamishwa rasmi mnamo mwaka wa 201. Hata hivyo, Vatikani ilijaribu mara mbili kumwondoa askofu halali wa Shantou, Monsignor Zhuang Jianjian, ili nafasi yake ichukuliwe na Huang
Wa pili alikuwa askofu ambaye aliteuliaa kwa njia haramu Guo Jincai wa Chengde. Vatikani ilisema wakati huo kuwa dayosisi ya Chengde haikuwem. Guo ndiye Katibu Mkuu katika baraza la Maaskofu ambalo hudhibitiwa na Serikali
Wa tatu ni Askofu Fang Jianping. Alitawazwa kwa njia haramu, na licha ya kutokuwa na majuto, baadaye alisamehewa na Vatikani. Baada ya kusamehewa alihusika tena katika utawazaji haramu wa kichungaji mara tat. Juma lililopita Fang alisema kuwa "uraia unastahila kuja mbele ya dini na …More
sw.news
21

Askofu Ambaye Alitia Sahihi Uamuzi Wa Kazakhstan Aadhibiwa?

Juma Lililopita Askofu Msaidizi Marian Eleganti, ambaye alikuwa mkuu wa watawa wa shirika la Benedict zamani, alijiuzulu kama aliye na wajibu wa vijana katika baraza la Maaskofu Waswizi huku akisema …More
Juma Lililopita Askofu Msaidizi Marian Eleganti, ambaye alikuwa mkuu wa watawa wa shirika la Benedict zamani, alijiuzulu kama aliye na wajibu wa vijana katika baraza la Maaskofu Waswizi huku akisema kuwa hakupata usaidizi kutoka kwa Maaskofu wengine. Eleganti aligonga vichwa vya habari kimataifa alipotia sahihi uamuzi wa Kazakhstan dhidi ya Amoris Laetitia mnamo mwezi Februari.
Sababu ya kujiuzulu kwake: Maaskofu hao walikuwa wameamua baada ya idhinisho la Eleganti kumtuma Askofu Msaidizi wa Fribourg Alain de Raemy, ambaye alikuwa kazizi wa jeshi la Uswizi hapo awali kwenye "Sinodi la vijana" mnamo mwezi Oktoba.
Hata hivyo Eleganti alitarajia kuteuliwa kuwa wa akiba lakini badala yake maaskofu hao walimteua mku wa watawa mhuria Urban Federer wa Einsiedeln ambaye ni mwanachama wa baraza hilo la maaskofu. Eleganti aliliona jambo hili kama kura ya kukosa imani na kujiuzulu.
Picha: Marian Eleganti, © Liebermary, Wikicommons, CC BY-SA, #newsDasrujcdey
sw.news
49

Marekebisho Ya Vatikani Ya Kifedha "Yamekufa"

Marekebisho ya Vatikani "yamekufa, yamekoma, yameisha". "Yamezuiliwa", msemaji mlei ambaye hakujitambulisha alimwambia Edward Pentin akiandika kwenye mtandao wa ncregister.com (Machi 12). Kulingana …More
Marekebisho ya Vatikani "yamekufa, yamekoma, yameisha". "Yamezuiliwa", msemaji mlei ambaye hakujitambulisha alimwambia Edward Pentin akiandika kwenye mtandao wa ncregister.com (Machi 12).
Kulingana na msemaji huyo wpinzani wa marekebisho hayo "wameyakomesha kabisa na watadanganya endapo wataulizwa".
Maadui wa marekebisho hayo walichangia katika mauti ya Kadinali Pell na kusababisha kusimamishwa kazi kwa Libero Milone kama "adui nambari moja wa raia".
Sekretarieti ya Uchumi ya Pell ilifichua kiasi kikubwa cha pesa ambacho hakikuwa kimerekodiwa kwenye nakala za fedha, Uro milioni 94 katika Sekretarieti ya masuala ya nchi za kigeni na takriban Uro bilioni 1 katika mashirika mengine.
Picha: © Zoe Toseland, CC BY-NC, #newsFsmzjdouyt
sw.news
44

Francis: Kadinali Lehmann "Alielekeza Maisha Ya Kanisa La Ujerumani [Lililokuwa Likifa]

Kadinali Karl Lehmann wa Mainz ambaye aliaga dunia mnamo tarehe 11 mwezi Machi, "alisaidia katika kuelekeza maisha ya Kanisa", Papa Francis aliandika kwenye telegramu. Kulingana naye, " roho yake Lehmann …More
Kadinali Karl Lehmann wa Mainz ambaye aliaga dunia mnamo tarehe 11 mwezi Machi, "alisaidia katika kuelekeza maisha ya Kanisa", Papa Francis aliandika kwenye telegramu. Kulingana naye, " roho yake Lehmann ilikuwa wazi kwa maswali na changamoto za nyakati".
Lehmann alianza kuiongoza Dayosisi ya Mainz mnamo mwaka wa 1983 wakati ambao Dayosisi hiyo ilikuwa na takriban Wakatoliki milioni moja na makasisi 50. Aliondoka mnamo mwaka wa 2016 Dayosisi hiyo ikiwa na Wakatoliki 740,000 na makasisi 396.
Lehmann alikuwa rafiki wa walio matajiri na wenye nguvu za kidunia kama vile Jean-Claude Juncker, Angela Merkel na wengine wengi. Walimtuza kwa angalau tuzo 31, miongoni mwake kukiwa na Medali ya Martin-Luther ambayo kwa kweli aliihitaji.
Kuwa wazushi wawili wajulikanao, Lehmann na Walter Kasper walifanya wakadinali mnamo mwezi Februari mwaka wa 2001 husababisha kivuli cha giza juu ya usia wa John Paul II.
Picha: Karl Lehmann, © Raimond Spekking, CC BY-SA, #newsTbhdmtsdqz
sw.news
21

Benedict XVI Huona Mwendeleo Na Francis, "Mwanaume Wa Msingi Mkuu Wa Kiteolojia"

Kadinali mstaafu Benedict XVI amemwandikia barua Monsignor Dario Edoardo Viganò kuhusiana na msururu wa vitabu 11 viitwavyo “Theology of Pope Francis” (Teolojia ya Papa Francis). Barua hiyo iliwasilishwa …More
Kadinali mstaafu Benedict XVI amemwandikia barua Monsignor Dario Edoardo Viganò kuhusiana na msururu wa vitabu 11 viitwavyo “Theology of Pope Francis” (Teolojia ya Papa Francis). Barua hiyo iliwasilishwa mnamotarehe 12 mwezi Machi, mtandao wa vaticannews.va umeandika.
Kwenye barua hiyo Benedict XVI alimwita Francis "mwanaume wa teolojia na msingi kuu wa falsafa", ingawaje yeye, Benedict, angekuwa tu "mtu wa makisia na teolojia aliye na ufahamu mchache wa maisha dhabiti ya Wakristu wa sasa".
Kulingana na Benedict XVI kuna "mwendeleo kati ya mapap wote wawili" licha ya "tofauti katika utaratibu na mienendo".
Picha: © mazur/catholicnews.org.uk CC BY-NC-SA, #newsAquxdavodl
sw.news
11

"Ushambulizi Wa Francis Dhidi Ya Useja Hufuata Ratiba Fulani"

Papa Francis anataka kulibadilisha Kanisa kwa mchakato wa polepole ili kuzuia utengano ambao unaeza kutokana na mbinu ya kustua na kuhofisha, kulingana na mwanahabari Mjerumani Müller-Meiningen. …More
Papa Francis anataka kulibadilisha Kanisa kwa mchakato wa polepole ili kuzuia utengano ambao unaeza kutokana na mbinu ya kustua na kuhofisha, kulingana na mwanahabari Mjerumani Müller-Meiningen.
Akiandika kwenye mtandao wa zeit.de (Machi 9), alieleza kuwa Francis ni "mjuzi mwenye busara" ambaye tayari aliingiza Ekaristi kwa wazini na analenga "kushambulia useja", "Matayarisho ya kutekeleza hili hayajafichwa kamwe, ila yanafuata ratiba thabiti."
Mjadala wa kwanza dhidi ya useja utakuwa wakati wa Sinodi la Vijana linalokuja mnamo mwezi Oktoba mwaka wa 2018 a kisha mjadala mkuu utakuwa katika Sinodi la Amazon. mnamo mwaka wa 2019.
Kulingana na Müller-Meiningen, "kitimbi" cha Francis kinahusisha kufutilia mbali tabia kwa kuzipuuza katika "kesi binafsi". Hili linaweza kutumika pia kwa shoga, upangaji uzazi bandia na mashemasi wa kike.
Picha: © Mazur, thepapalvisit.org.uk, CC BY-NC, #newsQgadmsyohs