sw.news
42

Afisa Wa Polisi Aliyeuawa Alikuwa Amebadili Dini Na Kuwa Mkatoliki

Usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi (Machi 23/24), Arnaud Beltrame, 45, afisa wa polisi Mfaransa mwenye cheo cha luteni kanali, aliaga dunia kutokana na majeraha ambayo aliyapata wakati wa oparesheni dhidi …More
Usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi (Machi 23/24), Arnaud Beltrame, 45, afisa wa polisi Mfaransa mwenye cheo cha luteni kanali, aliaga dunia kutokana na majeraha ambayo aliyapata wakati wa oparesheni dhidi ya magaidi.
Alikua amejitoa kama mateka kwa kuchukua nafasi ya mwanamke ambaye alikuwa ameshikwa na gaidi Radouane Lakdim kama mateka wa mwisho katika duka la Super U huko Trebes.
Beltrame alikuwa na matumaini ya kujadiliana na Lakdim baada ya wanunuzi hamsini na wafanyikazi ambao walijikuta kwenye shambulizi hilo kupelekwa pahali salama.
Lakini Lakdim, ambaye alikiri utiifu wake kwa Islamic State, alimpiga risasi na kumdunga, jambo lililowafanya polisi kushambulia na kumwua mshambulizi huyo.
Tayari Betrame alikuwa amekamilisha masaa 30 ya matayarisho ya ndoa yake ya kidini na Marielle, daktari wa wanyama, ambaye walikuwa wakiishi pamoja katika ndoa ya kimila bila watoto. Sherehe hiyo ilikuwa imeratibiwa kufanyika mwezi Juni.
Alipokea desturi zake za mwisho za dini kutoka kwa Padre Jean …More
sw.news
27

Hünermann Atuzwa Shahada Ya Heshima Ya Doctor Honoris Causa Katika Chuo Kikuu Cha Argentina

Mwanateolojia alipingalo Kanisa Katoliki Padre Peter Hünermann ambaye alikashifiwa na Benedict XVI kwenye barua ya hivi maajuzi, alituzwa shahada ya heshima, Doctor Honoris Causa, Katika chuo cha …More
Mwanateolojia alipingalo Kanisa Katoliki Padre Peter Hünermann ambaye alikashifiwa na Benedict XVI kwenye barua ya hivi maajuzi, alituzwa shahada ya heshima, Doctor Honoris Causa, Katika chuo cha Kichungaji cha Universidad Católica Argentina mnamo mwaka wa 20004 wakati ambapo Jorge Mario Bergoglio alikuwa Chansela mkuu.
Msimamizi katika chuo hicho wakati huo alikuwa Padre Alfredo Zecca ambaye msimamizi wake katika masomo ya Shahada ya uzamivu alikuwa Hünermann. Baadaye Zecca alifanywa askofu mkuu wa Tucumán hadi alipofutwa kazi na Papa Francis mnamo mwezi Juni mwaka wa 2017.
Hünermann alikuwa akifunza nchini Argentina katika mradi uliokuwa ukilenga kueneza teolojia chafu ya Ujerumani katika Amerika Kusini.
Alipokuwa akifunza huko Buenos Aires alikuwa akiishi katika seminari ya Wayesu ambapo Bergoglio alikuwa mkuu wa wanafunzi. Hivyo basi, kwa miaka mingi, wawili hao walikutana mara nyingi.
Picha: Pontificia Universidad Católica Argentina, © wikicommons, CC BY-SA, #newsYczzlsvjbk
sw.news
20

Gloria.tv: Kama Mnavyoona, Malengo Yetu Yako Juu

Tangu msimu wa kiangazi uliopita Gloria.tv imeongeza idadi ya watumizi wake. Hivi sasa sisi huchapisha habari katika lugha kadhaa. Hili husababisha msongo kwenye sava zetu. Mnamo mwaka wa 2017 hatukua …More
Tangu msimu wa kiangazi uliopita Gloria.tv imeongeza idadi ya watumizi wake. Hivi sasa sisi huchapisha habari katika lugha kadhaa. Hili husababisha msongo kwenye sava zetu. Mnamo mwaka wa 2017 hatukua na budi ila kulipa zaidi ya dola 30, 000 kugharamia kompyuta za sava, ufuasi na stima katika vituo kadhaa vya data. Hizi ni pesa nyingi kwetu - lakini chache ikilinganishwa na kiasi cha uhubiri wa Gloria.tv.
Gloria.tv imeendelea kukua licha ya mikakati amilifu kwenye mitandao ya kijamii na mitandao ya kutafuta kubagua dhidi ya maudhui ya Kikatoliki na yale ya kihifidhina. Tuliona hili tangu msimu wa kiangazi uliopita - muda mrefu kabla ya vyombo vya habari kuanza kuzungumza kuhusu jitihada hizi - kwamba tulikuwa tukipoteza wafuasi kutoka kwao. Lakini tumeweza kufidia na kukua.
Kiasi kikubwa cha fedha zetu hutokana na barua za uchangishaji wa pesa. Tunatumaini na kuomba kwamba kupitia kwa kampeni hii ya mtandaoni ya msimu huu wa Kwaresima tutapokea dola 10,000 zaidi. Kufikia sasa tumeweza …More
sw.news
15

Wasilisho La Kitabu Cha Mahojiano Cha Francis - Hakuna Aliyehudhuria

Ni watu 25 tu ndio walihudhuria wasilisho la kitabu kipya cha mahojiano cha Papa Francis, "God is Young" kulingana na kituo ambacho humuunga Francis mkono IlFattoQuotidiano (March 23). Francis …More
Ni watu 25 tu ndio walihudhuria wasilisho la kitabu kipya cha mahojiano cha Papa Francis, "God is Young" kulingana na kituo ambacho humuunga Francis mkono IlFattoQuotidiano (March 23).
Francis alikiandika kitabu hicho pamoja na mwanahabari wa anzilisho la Italia Thomas Leoncini. Kilichapishwa na Piemme kwa ushirikiano na maktaba ya Vatikani.
Tukio hilo lilifanyika katika chuo kikuu cha Augustinianum kilicho karibu na Vatikani.
Hakuna Kadinali na Askofu wa utawala wa Roma aliyekuwa amehudhuria.
#newsLrkakyhfxl
sw.news
18

Benedict XVI Alikuwa Amekubali Kuchapishwa Kwa Sehemu Ya Barua Yake

Chapisho la sehemu ya barua ya kibinafsi ya Benedict XVI kwa Monsignor Dario Viganò lilikuwa limekubaliwa, Padre Myesu wa Ujerumani Bernd Hagenkord ameandika. Hagenkord ndiye mhariri mkuu wa sehemu …More
Chapisho la sehemu ya barua ya kibinafsi ya Benedict XVI kwa Monsignor Dario Viganò lilikuwa limekubaliwa, Padre Myesu wa Ujerumani Bernd Hagenkord ameandika.
Hagenkord ndiye mhariri mkuu wa sehemu za lugha sita za VaticanNews na mshirika wa karibu wa Viganò.
Kwenye kauli katika blogu lake mnamo tarehe 22 mwezi Machi, Hagenkord anasisitiza kwamba hakukuwa na udanganyifu wala utumizi mbaya kuhusiana na kitendo cha Viganò.
Kauli hii ina maana kwamba Viganò alijitia kwenye maji moto baada ya kuchapisha barua kamili ingawaje hakuwa na idhini ya kufanya hivyo. Bila shaka hangeweza kustahimili shinikizo kutoka kwa vyombo vya habari bandia. Hili lilimsababishia Benedict XVI mafadhaiko kwani Viganó alifichua sura mbili za papa huyo wa kitambo.
Kwenye barua yake ya kibinafsi Benedict anamshambulia mwanateolojia ambaye hulipinga Kanisa Katoliki, Padre Peter Hünermann ingawaje hadharani Hünermann alikuwa miongoni mwa wahariri wa kitabu cha mwaka wa 2005 ambacho kilikuwa na sehemu tatu zilizochangiwa …More
sw.news
44

Francis Huwa Hawaondoi Kutokana Na Ukosefu Wa Maarifa - Basi Ni Kwa Nini Viganò Hakuwa Na Budi Ila Kuondoka

Hatima ya Monsignor Dario Viganò ni tofauti na hatima ya wachungaji wengine walioko kwenye taabu, mfuasi wa Francis John Allen ameandika kwenye mtandao wa cruxnow.com (Machi 22). Amesema kwamba kwa …More
Hatima ya Monsignor Dario Viganò ni tofauti na hatima ya wachungaji wengine walioko kwenye taabu, mfuasi wa Francis John Allen ameandika kwenye mtandao wa cruxnow.com (Machi 22).
Amesema kwamba kwa kawaida Francis husimama na aliowachagua, kila wanaposhambuliwa.
Allen alimtaha Askofu wa Chile Juan Barros ambaye alikashifiwa kwa kusemekana kuwa alisetiri dhulma za kijinsia, na Monsignor Gian Battista Ricca, Askofu aliye na cheo kikuu katika benki ya Vatikani na aliye Mkurugenzi wa Casa Santa Marta, ambaye hapo awali alikuwa na mashida na tabia za kishoga.
Hivyo basi swali ni kwa nini Viganò hakuwa na budi ila kuondoka
Picha: Dario Viganò, © Associazione Amici di Piero Chiara, CC BY, #newsMejwguhapz
sw.news
24

Hata Wafuasi Wa Francis Wanajua Kwamba "The Dictator Pope" Ni Kweli

Henry Sire, mwandishi wa kitabu cha The Dictator Pope, ambaye tangu kuchapishwa kwa jina lake uanachama wake kwenye shirika la Knights of Malta umebatilishwa, ameyapinga madai ya Maaskari hao kwamba …More
Henry Sire, mwandishi wa kitabu cha The Dictator Pope, ambaye tangu kuchapishwa kwa jina lake uanachama wake kwenye shirika la Knights of Malta umebatilishwa, ameyapinga madai ya Maaskari hao kwamba kitabu chake ni "shambulizi ovu" dhidi ya Francis.
Kwenye barua pepe kwa shirika la habari la AP Sire alisema kwamba yeye huulinda utakatifu wa ofisi ya Papa dhidi ya aliyeishikilia ofisi hiyo ambaye, kama waonavyo Wakatoliki wengi sasa, "bila shaka hupungukiwa na nafsi ambayo hutarajiwa katika papa kwa karne nyingi".
Shirika la AP limesema kwamba kwa wakati mwingine Sire hutoa taswira mbaya ya Francis ingawaje linakiri kwamba hata wafuasi wa Francis husema kwamba "huwa na kiasi fulani cha ukweli".
#newsHwbsgarafr
sw.news
23

Dayosisi Ya Ufaransa Yabadilisha Kanzu Kuwa Suruali Ya Patashika

Dayosisi tatu za Ufaransa za Perpignan, Montpellier na Nimes zimetumia picha ya Kasisi ambaye amevalia kanzu ambayo imeundwa hivi kwamba ilionekana kana kwamba kasisi huyo alikuwa amevalia suruali ya …More
Dayosisi tatu za Ufaransa za Perpignan, Montpellier na Nimes zimetumia picha ya Kasisi ambaye amevalia kanzu ambayo imeundwa hivi kwamba ilionekana kana kwamba kasisi huyo alikuwa amevalia suruali ya patashika.
Kulingana na Le Salon Beige (Machi 19) picha hiyo ilitumika kwenye kampeni ya kuchangisha pesa.
#newsFzvnmorkmg
sw.news
19

Mustakabali Wa Kanisa Ni Ibada Ya Kale Ya Kilatini

Ibada ya Kale ya Misa ya Kilatini huwavutia vijana wengi kwa sababu huwa inawapa changamoto, Bertlan Kiss alisema, Rais wa Mhungaria wa shirika la vijana Foederatio Internationalis Juventutem ambaye …More
Ibada ya Kale ya Misa ya Kilatini huwavutia vijana wengi kwa sababu huwa inawapa changamoto, Bertlan Kiss alisema, Rais wa Mhungaria wa shirika la vijana Foederatio Internationalis Juventutem ambaye kwa sasa yuko Roma kama mjumbe katika mkutano wa matayarisho ya Sinodi.
Akizungumza na ncregister.com (Machi 21), Kiss alieleza kwamba vijana hupendelea Ibada ya Kale kwa sababu inahusiana na utumizi wa hazina na uridhi wote wa Kanisa kuokoa nyoyo.
Kiss alimsifu Papa Francis kwa kutaja neno "mizizi" wakati wa mkutano wa matayarisho ya sinodi. Kulingana na Kiss hili linamaanisha kwamba Francis "anasisitizia Tamasuni". Ana imani kwamba anaweza kubadilisha mtazamo wa maaskofu na makadinali kwa kukutana kibinafsi na kwa "kulitenganisha na siasa" suala la litajia. Hata hivyo, huenda watu walijaribu mbinu hii kabla yake.
Picha: © Matthew Doyle, CC BY-ND, #newsZpsyukustu
sw.news
23

Viganò Aondoka

Papa Francis amekubali kujiuzulu kwa Msgr. Dario Viganò kama kinara wa Afisi ya Mawasilia no. Nafasi yake imechukuliwa na Msgr Adrian Ruiz, aliyekuwa mkuu wa Vatican Internet Service (Huduma za Intaneti …More
Papa Francis amekubali kujiuzulu kwa Msgr. Dario Viganò kama kinara wa Afisi ya Mawasilia no.
Nafasi yake imechukuliwa na Msgr Adrian Ruiz, aliyekuwa mkuu wa Vatican Internet Service (Huduma za Intaneti za Vatikani).
Hili limekuja baada ya Viganò kuchapisha na kubadilisha barua aliyokuwa ameipokea kama jibu kutoka kwa Benedict XVI.
Sababu halisi ya kujiuzulu kwa Viganó ingawaje haijabainika wazi kwani ndani ya Vatikani kutoweza kufanya kazi kamwe hakujakuwa sababu ya kuwaachisha kazi watu ambao huwainamia wakuu wao.
Papa Francis sasa amemtangaza Viganò kuwa "mshauri" katika Afisi ya Mawasiliano ambayo Viganò amekuwa kinara wake hadi leo.
Picha: Dario Viganò, © Associazione Amici di Piero Chiara CC BY-SA, #newsFnxczitdiz
sw.news
18

Maaskofu Wajerumani Wamtumia Kasisi Aliyetanguka Kueneza Chuki Dhidi Ya Benedict XVI

Mtandao wa masskofu Wajerumani katholisch.de ulichapisha mnamo tarehe 21 mwezi Machi - sikukuu ya Mtakatifu Benedict - nakala ya kuchukiza dhidi ya Benedict XVI ambayo iliandikwa na mwandishi wa habari …More
Mtandao wa masskofu Wajerumani katholisch.de ulichapisha mnamo tarehe 21 mwezi Machi - sikukuu ya Mtakatifu Benedict - nakala ya kuchukiza dhidi ya Benedict XVI ambayo iliandikwa na mwandishi wa habari mtetezi ushoga Joachim Frank, kasisi ambaye alitanguka.
Anaipuuza barua ya kibinafsi ya Francis ambayo ilifichuliwa juma lililopita na kuvutwa kwa hila na aliyekuwa mkuu wa zamani wa vyombo vya habari wa Vatikani Monsignor Dario Viganò ili kutoa taswira ya "ufungamano" kati ya Benedict na Francis.
Frank alisema katika nakala hiyo kwamba yeye binafsi "amekasirishwa". Alimtukana Benedict kuwa "Panzerkardinal" [samaki wa tenki] huku akimkashifu kwa kuwa "mgumu" na "mwenye kisasi" kwani katika barua hiyo ya kibinafsi alieleza shaka zake dhidi ya mwanateolojia Mjerumani ambaye hulipinga Kanisa Katoliki vikali Padre Peter Hünermann ambaye Francis alimpokea faraghani mnamo mwezi Mei mwaka wa 2015.
Maoni ya watumizi kwenye mtandao wa katholisch.de walikosoa mtandao wa Maaskofu hao kwa sababu …More
sw.news
26

Caritas Ilihusika Katika Utunzi Wa Mwongozo Wa Kuendeleza Upangaji Uzazi

Caritas Internationalis, shirika la msaada la Vatikani, limo kewenye bodi ya wakurugenzi ya The Sphere Project ambayo madhumuni yake ni kusambaza kijitabu ambavyo vinaendeleza upangaji uzazi na homoni …More
Caritas Internationalis, shirika la msaada la Vatikani, limo kewenye bodi ya wakurugenzi ya The Sphere Project ambayo madhumuni yake ni kusambaza kijitabu ambavyo vinaendeleza upangaji uzazi na homoni za uavyaji mimba katika kurasa kadhaa. Kashfa hii ilifichuliwa na Taasisi ya Lepanto (Machi 20).
Kijitabu hicho kinaeleza "kanuni za msaada wa maendeleo". Ni jambo la kawaida kwa wanachama wa Caritas Internationalis ambalo lilishiriki katika utunzi na usahihishaji wa nakala hiyo.
Kijitabu hicho kinawataka wafanyikazi wa msaada kujua kuhusu "huduma za upangaji uzazi" na kudai kuwa ni "muhimu" kupata mipira ya kondomu bila malipo. Toleo lake la mwaka wa 2011 limeorodhesha "Kondomu za bure za wanaume na kondomu za bure za wanawake" miongoni mwa "huduma muhimu za afya".
Baadhi ya toleo za kitabu hicho zi tanbihi inayosema kuwa Caritas Internationalis "haiendelezi matumizi ya, au kusambaza aina yoyote ya, upangaji uzazi bandia." Kulingana na Mafundisho ya Kikatoliki, utumizi wa upangaji …More
sw.news
28

Mwanateolojia wa Maadili: Francis Analielekeza Kanisa Kwenye "Janga La Kiroho"

Kinachoitwa "dhana mpya" zinazotokana na Amoris Laetitia, zinapendekeza kwamba baadhi ya Wakatoliki hawatakikani kutii sheria takatifu na za asili, Christian Brugger, baba wa watoto watano ambaye alifunza …More
Kinachoitwa "dhana mpya" zinazotokana na Amoris Laetitia, zinapendekeza kwamba baadhi ya Wakatoliki hawatakikani kutii sheria takatifu na za asili, Christian Brugger, baba wa watoto watano ambaye alifunza teolojia ya maadili na kutumikia kama mshauri wa kiteolojia wa maaskofu wa Marekani, aliandika kwenye mtandao wa ncregister.com (Machi 19).
Brugger anawaomba maaskofu hao kuzipinga "dhana hizi mpya" ambazo maarifa yake "kwa uhakika yatatumika katika vitendo vya upangaji uzazi bandia, tabia za kishoga, na katika tabia zingine zilizokatalika kitamaduni".
Ana imani kwamba ni uamuzi wa aina hiyo tu ndio ambao unaweza kubadilisha ambacha kwa sababu nyingine kitakuwa "janga la kiroho kwa Kanisa Katoliki." Kama sivyo "maovu makuu yatafanyika na nyoyo nyingi zitapotea", Brugger anaonya.
Picha: © Mazur, catholicchurch.org.uk, CC BY-NC-SA, #newsWkyaepnifd
sw.news
30

Francis Ana Mpango - Huenda Ukawa "Mdanganyifu"

Ross Douthat aliandika kwamba Papa Francis hufuata "mpango" ambao unaweza kuonekana kuwa mnyofu au ulio mdanganyifu. Akiandika kwenye gazeti la New York Times (Machi 16), Douthat alisema kwamba Francis …More
Ross Douthat aliandika kwamba Papa Francis hufuata "mpango" ambao unaweza kuonekana kuwa mnyofu au ulio mdanganyifu.
Akiandika kwenye gazeti la New York Times (Machi 16), Douthat alisema kwamba Francis "habadilishi rasmi" mafunzo ya Kanisa juu ya talaka, na kufunga ndoa tena, ndoa kati ya watu wa jinsia sawa na kifo cha huruma, huku akiongeza kuwa mabadiliko ya aina hiyo yamepita nguvu za ofisi yake.
Lakini Francis hutoa tofauti [za kustaajabisha] kati ya mafundisho na kazi ya uchungaji huku akidai kuwa mtu anaweza kuibadilisha kazi ya uchungaji na kuuacha ukweli wa mafundisho ulivyo. Hivyo basi mzini anaweza kupokea Ekaristi, Mkatoliki aliyeuawa kifo cha huruma anaweza kupokea ibada zake za mwisho na shoga kubarikiwa ndoa yake.
Kulingana na Douthat, Francis anaonekana kuamini kwamba hakuna baadhi ya hayo ambayo hubadilisha mafunzo ya Kanisa [lakini kwa kweli hubadilisha].
Picha: © Mazur, catholicnews.org.ukCC BY-NC-SA, #newsJplfukqwlt
sw.news
40

Mwandishi Wa ‘The Dictator Pope’ Afichuliwa (Video Ya Kipekee)

Mwandishi wa kitabu kizuri cha Dictator Pope amefichuliwa kuwa mwanahistoria Henry Sire, kulingana na Catholic Herald (Machi 19). Sire alikichapisha kitabu chake mnamo mwezi Desemba chini ya jina …More
Mwandishi wa kitabu kizuri cha Dictator Pope amefichuliwa kuwa mwanahistoria Henry Sire, kulingana na Catholic Herald (Machi 19).
Sire alikichapisha kitabu chake mnamo mwezi Desemba chini ya jina Marcantonio Colonna. Alizaliwa mnamo mwaka wa 1949 mjini Barcelona na hivi sasa yeye huishi Rome anakofanya kazi kama mwanahistoria. Ana shahada katika Historia ya Kisasa kutoka chuo kikuu cha Oxford.
Sire ni mgeni katika mkutano wa msimu wa kiangazi wa kila mwaka wa Baraza la Kikatoliki la Rome mjini Gardone, nchin Italia.
Picha: Henry Sire, © Joseph Shaw, CC BY-NC-SA, #newsEhgpwprhqx
sw.news
26

Francis Awabembeleza "Vijana" Bandia Wa Mrengo Wa Kushoto

Kwa kauli yake ya kawaia ya "Zungumza kwa ujasiri, usione aibu", Papa Francis alihutubia mkutano wa matayarisho ya sinodi uliokuwa umehudhuriwa na wapinduzi 300 wakali wa mrengo wa kushoto ambao …More
Kwa kauli yake ya kawaia ya "Zungumza kwa ujasiri, usione aibu", Papa Francis alihutubia mkutano wa matayarisho ya sinodi uliokuwa umehudhuriwa na wapinduzi 300 wakali wa mrengo wa kushoto ambao walichaguliwa na kualikwa na Francis ili kuwawakilisha "vijana". Wakati wa mkutano wao wa kwanza mnamo tarehe 19 mwezi Machi huko Rome, aliwaambia wasema "wanachohisi".
Francis alitoa mwito kwa Kanisa liwasikilize "vijana" ambao yeye mwenyewe hakuwachagua miongoni mwa Wakatoliki ila miongoni mwa watu wasiosadiki uwepo wa Mungu na wachukia serikali. Hivi, Francis anajaribu kuelewa anachokitaka "Mungu" kutoka kwa Kanisa "la leo".
Sio jambo la kushangaza kuwa mjumbe wa Australia Angela Markas aliambia mkutano huo wa matayarisho ya Sinodi kwamba anataka mjadala kuhusu jinsia, ndoa za kishoga na jukumu la wanawake, yaani masuala ya kawaida ambayo hukuzwa na vyombo vya habari vya kibiashara ambavyo hufaana nayo.
Mvatikani Cindy wooden aliandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba Francis alijibu swali …More
sw.news
26

Tunastahili Kushikamana - Kadinali Sarah

"Tukiishi peke yete, tutapotea" - Kadinali Robert Sarah aliwaambia wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kanada cha Mtakatifu Michael (Machi 12), "ni vigumu kudumisha imani yetu bila jamii". Gloria.tv ndichoMore
"Tukiishi peke yete, tutapotea" - Kadinali Robert Sarah aliwaambia wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Kanada cha Mtakatifu Michael (Machi 12), "ni vigumu kudumisha imani yetu bila jamii".
Gloria.tv ndicho kifaa cha mtandaoni cha Wakatoliki kuwasiliana.
Wakatoliki wanastahli kuwa na uhuru dhidi ya mitandao ya kijamii ambayo, hatimaye, huwachukia Wakatoliki na itafanya lolote iwezalo ili kuzuia utume wa kweli wa Kikatoliki. Wakatoliki wanahitaji mtandao huru wa kijamii.
Tafadhali, tusaidie wakati huu wa Kwaresima
Picha: Robert Sarah, © Antoine Mekary, Aleteia, CC BY-NC-ND, #newsMkatkqwkjg
sw.news
33

Schönborn Ana Imani Kwamba Francis Ni "Zawadi Kutoka Kwa Mungu" Kwake

Papa Francis ni zawadi kutoka kwa Mungu "kwangu na kwa wengi", Kadinali Schönborn wa Vienna ambaye ni mtetezi wa mashoga aliambia kituo cha televisheni ambacho hulipinga Kanisa Katoliki ORF (Machi 18). …More
Papa Francis ni zawadi kutoka kwa Mungu "kwangu na kwa wengi", Kadinali Schönborn wa Vienna ambaye ni mtetezi wa mashoga aliambia kituo cha televisheni ambacho hulipinga Kanisa Katoliki ORF (Machi 18).
Schönborn alikiri kuwa Francis anadhaminiwa zaidi "nje" ya Kanisa huku "baadhi ya vikundi Kanisani" [yaani Wakatoliki] huhofia kwamba Francis huwa - alichokiita Schönborn - "wazi sana".
Sehemu kubwa ya mahojiano hayo ilikuwa domo. Schönborn ana historia ya kumsifu Papa yeyote aliye mamlakani kwa shauku.
Picha: Christoph Schönborn © Mazur, catholicnews.org.uk, CC BY-SA, #newsJqdssuhjvn
sw.news
27

Hünermann Ambaye Hulipinga Kanisa Katoliki Aliitengenezea Nakala Ya Francis Amoris Laetitia Njia

Padre Mjerumani Peter Hünermann, mwanateolojia ambaye hulipinga Kanisa Katoliki aliyekashifiwa na Benedict XVI katika barua ya kibinafsi ya hivi maajuzi, alipokelewa na Papa Francis mnamo mwezi Mei …More
Padre Mjerumani Peter Hünermann, mwanateolojia ambaye hulipinga Kanisa Katoliki aliyekashifiwa na Benedict XVI katika barua ya kibinafsi ya hivi maajuzi, alipokelewa na Papa Francis mnamo mwezi Mei mwaka wa 2015 kwa muda wa takriban saa moja katika mji wa Santa Marta.
Kulingana na mtandao wa commonwealmagazine.org (Septemba 22, 2016), Hünermann "ushawishi mkubwa wa kiteolojia" ambao huenea hadi kwa nakala ya Francis Amoris Laetitia na kumpa Francis "kisingizio cha kiteolojia" kwa kuingiza talaka Kanisani kwa vitendo.
Hünermann aliambia commonwealmagazine.org kwamba nakala ya Amoris Laetitia huwafungulia mlango wazini kupokea Ekaristi. Aliongeza kwamba sula la mashemasi wa kike "lina umunimu mwingi kwangu kwa zaidi ya miaka arobaini".
#newsDhwgjseuhj
sw.news
12

Mashirika Ya Kisiri Hulitumia Kanisa Kuu La Munich Kufanya Upelelezi

Shirika la ukachero la serikali ya muungano ya Ujerumani lilitumia Kanisa Kuu la Munich kufanya upelelezi, jarida la kila juma ambalo hupinga Kanisa Katoliki Spiegel limetangaza. Katika miaka ya …More
Shirika la ukachero la serikali ya muungano ya Ujerumani lilitumia Kanisa Kuu la Munich kufanya upelelezi, jarida la kila juma ambalo hupinga Kanisa Katoliki Spiegel limetangaza.
Katika miaka ya themanini shirika hilo liliweka vifaa vyake kwenye minara ya kengele ya Kanisa hilo ili kupokea na kutuma data. Ajenti wa shirika hilo mwenye maarifa mengi alisema kuwa kuna shirika lingine pia ambalo lilitumia Kanisa hilo kulingana na Spiegel "na pengine hulitumia hadi wa leo".
Dayosisi kuu ya Munich ilikiri kuwa katika mnamra wa Kaskazini kuna "baadhi ya vifaa vya mashirika tofauti".
Picha: Liebfrauendom München, © digital cat, Flickr, CC BY, #newsLjfmkirthn